- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo
(aliyesimama) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi
ya Ardhi (NLUPC) Dkt. Stephen Nindi wakiongoza kikao cha pamoja kati ya NLUPC
na TFS juu ya maandalizi ya upangaji wa mipango ya matumizi ya ardhi katika
vijiji vinavyozunguka hifadhi za Misitu inayosimamamiwa na Serikali Kuu.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu, Sera na Mawasiliano (DLCCP) wa Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi ya Ardhi, Bibi Albina Burra (kulia) pamoja na Watalamu wa Wakala wa
Huduma za Misitu (TFS) wakifuatilia kwa maokini mazungumzo kati ya taasisi zao.
Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
(NLUPC) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
inatarajia kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 120 vinavyozunguka
misitu ya Hifadhi ya Serikali Kuu.
Akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya
NLUPC and TFS kilichofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NLUPC
Dkt. Stephen Nindi ameahidi kuwa taasisi yake itatoa ushirikiano wa kitaalamu
kwa ajili ya kunusuru rasilimali za nchi wakati wowote kwa faida ya nchi na
watanzania wote.
Naye Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos
Silayo amesema kuwa mipango hiyo ya matumizi ya ardhi inalenga kumaliza changamoto zote ya kuhifadhi misitu
nchini kwenye vijiji vinavyozunguka hifadhi hizo pamoja na kuwasaidia
wanavijiji kuwa na matumizi rafiki ya ardhi yatakayosaidia kutunza misitu hiyo.
“Mpaka sasa zaidi 60% ya misitu iliyopo nchini
haijahifadhiwa na lengo letu ni kuhakikisha misitu hiyo inahifadhiwa. Hivyo nawataka
wataalamu wa Tume pamoja na Wakala kuhakikisha lengo hili linafikiwa kwa kuweka
mikakati ya kitaaaluma kwa kuzingatia wakati uliopo,” alisema Professa Silayo.
Professa Silayo anasema
hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayoelekeza kutatua migogoro
ya mipaka kati ya wananchi na maeneo ya jirani na hifadhi kwa kushirikisha
wadau katika kuhakiki mipaka ya maeneo ya hifadhi kwa kuweka alama za kudumu;
kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi; na kuzingatia utawala wa Sheria
katika kusimamia rasilimali za maliasili.
Mtendaji huyo anaongeza kuwa uharibifu wa
misitu nchini ni mkubwa katika maeneo ambayo vijiji vimeanzishwa ndani ya
misitu bila kufuata sheria na TFS imeendelea kuzuia upanuzi zaidi wa vijiji
hivyo, na hadi sasa kuna vijiji 228 vinavyofahamika na miji kadhaa.
NLUPC na TFS wameunda kikosi kazi
kitakachoandaa mikakati ya namna bora ya kufanya kazi hiyo ambapo wameanza kwa
kupitia orodha ya misitu ya hifadhi yenye migogoro kwa kanda zote saba za TFS.
Kanda hizo ni za Mashariki, Kaskazini, Kati, Kusini, Nyanda za juu Kusini, Ziwa
na Magharibi.
Comments
Post a Comment