- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi wa
Kata ya Mkata wilayani Handeni wakati wa ziara yake ya kutembelea na
kukagua miradi ya Maji inayotekelezwa.
MKUU
wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe katika akimueleza jambo Naibu Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia wakati wa ziara hiyo kushoto
ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe mara baada ya kutembelea
mradi wa Maji eneo la Mkata katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa
wilaya ya Handeni William Makufwe
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimsikiliza kwa
umakini Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita wakati wa
ziara hiyo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe.
Wakandarasi ambao Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso aliotaka wawekwe ndani wakiwa chini ya ulinzi
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wa pili kutoka kushoto akiwa
na Mkuu wa wilaya ya Handeni kulia wakati wakitembelea miradi ya maji
wilayani humo wakati wa ziara yake kulia ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa
wilaya ya Handeni William Makufwe kushoto ni Diwani wa Kata ya Mkata
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akiwa amepanda juu kwenye tenki eneo la mkata kulikagua wakati wa ziara yake
Naibu
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kushoto akilakiwa na
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe mara baada
ya kuwasili mjini Handeni
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akiwa na Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Mtendaji wa wilaya ya Handeni William Makufwe akimueleza
jambo Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso mara baada ya
kutembelea miradi ya maji kwenye eneo la Mkata katikati ni Mkuu wa
wilaya ya Handeni Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ameamuru kuwekwa ndani wakandarasi wanaotekelezwa mradi wa maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu eneo la mkata wilayani Handeni baada ya kushindwa kuwepo kwenye eneo la mradi licha ya kupewa taarifa za uwepo wa ziara yake.
Wakandarasi ambao walilazimika kuwekwa ndani ni Mkandarasi wa Kampuni ya Tansino Logistick Limited ya Dar Abdul Ismail na Charles Stephano ambaye ni mkandarasi wa ujenzi huku Chales Tarimbo mshauri Mkandarasi naye akikumbana na kadhia hiyo.
Agizo hilo alilitoa leo wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa kwenye kata ya Mkata wilayani Handeni ambapo miradi hiyo mitatu ilikuwa ikigharimu zaidi ya sh.bilioni tatu.
Akiwa kwenye eneo hilo Naibu Waziri huyo alisema haiwezekani wabunge wanaomba miradi ya maji na serikali inatenga lakini watu wachache wanatumia fedha hizo kwenye matumizi kwa maslahi yao binafasi na kuwafanya wananchi kuendelea kuteseka na tatizo la maji.
Alisema kutokana na kuwepo kwa tabia hiyo ambayo imekuwa ikirudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa serikali hawatavumiliwa badala yake watahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.
“Ndugu zangu wakati Rais akiniteua aliniagiza nihakikisha wananchi wanapata 1maji vinginevyo nitatumbuliwaa nami sipo tayari kwa hilo hivyo nitahakikisha tunawachukulia hatua kali wakandarasi wanaoshindwa kuendena na kasi na hivyo kuikwamisha kwa maslahi yao binafasi huku wananchi wakiendelea kuteseka”Alisema.
Naye kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini (CCM) Mboni Mhita alimuelezwa Naibu Waziri huyo kuwa mradi huo umejengwa chini ya kiwango na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka na adha ya maji.
“Mh Naibu Waziri wilaya ya Handeni ni miongoni mwa wilaya ambazo zinachangamoto kubwa ya tatizo la maji lakini sisi kama wabunge tumekuwa tukiiomba fedha za mradi ya maji lakini wakandarasi wamekuwa wakitukwamisha”alisema.
Alisema kinachofanywa na wakandasi hao juu ya utekelezaji wa miradi hii ni ubadhirifu wa wazi kabisa hivyo ili kuondokana na tatizo hilo serikali inapaswa kuwachukulia hatua wakandarasi wa namna hiyo ili iwe fundisho wa wengine wenye tabia za namna hiyo.
Naye kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe alisema miradi hiyo ambayo Rais aliagiza imalizike leo (jana)Julai 23 huku jambo la kushangaza hakuna dalili ya umalizikaji wa miradi hiyo. Miradi hiyo ambayo ilitakiwa kutelezwa Wilayani hapo ni pamoja na bwawa la mkata,bwawa la manga na miundombinu ya mambomba toka katika bwawa la mkata hadi mkata mjini jambo ambalo halijafanyika hadi mwisho wa agizo
Comments
Post a Comment