- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MOSCOW,
RUSSIA
NDEGE iliyowabeba
wachezaji wa timu ya taifa ya Saudi Arabia kuelekea kusini mwa Urusi, kwa
michuano inayoendelea imetua salama baada ya kupata hitilafu katika moja ya
injini ya ndege hiyo baada ya moto kutokea.
Picha za
video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaionyesha ndege hiyo katika
chini ya bawa lake kukiwa na cheche za moto.
Ndege hiyo
ya shirika la Rossiya ilipatwa na shida hiyo wakati ikitua uwanja wa
Rostov-on-Don.
Shirikisho
la Soka la Saudia, limesema kuwa wachezaji wote wapo salama.
Mchezaji
kiungo wa Saudi Arabia Atan Bahbir, na mchezaji katika nafasi ya ulinzi Osama
Hawsawi, wanasema wanamshukuru Mungu kwa kuwafikisha salama.
"Tunashukuru
kwa swali lako, tunamshukuru Mungu, msafara mzima umefika salama. Kulikuwa na
shida ya kiufundi, na tulipatwa na uoga kidogo.
Naye
mchezaji Osama amesema kuwa wanashukuru Mungu kuona kwamba sasa wapo hotelini,
kwani kwa sasa kila kitu kipo sawa, na amesema wanamuomba Mungu washinde katika
mchezo wao.
Comments
Post a Comment