- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
LONDON,
UINGEREZA
UCHUNGUZI wa
mara kwa mara wa ziwa la mama ''unaweza kusababisha madhara kuliko faida'' na
kwa wanawake ambao hukosa uchunguzi huo wanastahili kuendelea na maisha yao, madaktari
wamesema.
Kundi la
madaktari wa afya 15 wameliandikia gazeti la the Times wakisema wanawake
hawastahili kuwekwa katika ''hali ya wasiwasi''
Hii ni
baada ya wanawake 450,000 kutoka England kukosa mualiko kwa uchunguzi huo wa
kila wakati kutokana na hitilafu za kompyuta.
Mashirika
ya kutoa msaada kwa wagonjwa wa saratani ya matiti wamesema mpango huo wa
uchunguzi unawapatia wanawake ''nafasi bora'' ya matibabu iwapo ugonjwa huo
utagundulika mapema.
'Hakuna tofauti'
Kwenye
barua hiyo kwa gazeti hilo, kikundi cha wasomi wamesema wanawake wenye umri wa
miaka 70-79 ambao huenda kufanyiwa uchunguzi huo wanastahili kutafuta usaidizi
iwapo watagundua wanauvimbe wowote ama dalili za ugonjwa huo.
"Wanawake
wengi na madaktari sasa wanajiepusha na uchunguzi huo kwa sababu hauna manufaa
yoyote ya kusababisha vifo."
Uchunguzi
huo wa matiti kwa mara nyingi husababisha madhara kuliko faida, jambo ambalo
limeanza kufahamika kimataifa.
Madai ya
kuyaokoa maisha ya watu kutokana na uchunguzi huo yanasawazishwa na vifo,
madaktari hao wamesema.
Na
saratani ambazo ni hatari na zilizo katika kiwango kibaya hazizuiliwi na mpango
huo wa uchunguzi , wamesema.
Miongoni
mwa waliotia saini barua hiyo ni Susan Bewley, profesa wa wanawake wa chuo cha
taasisi cha Kings, na Michael Baum profesa wa upasuaji wa chuo kikuu cha
London.
Makosa
yaliorodheshwa kutoka mwaka 2009 , yalitolewa wiki iliyopita. Wanawake 270
nchini Uingereza wamefariki kwa kukosa kurudi kwa uchunguzi kwa mara nyengine.
Wanawake
309,000 ambao walikuwa hai watatumiwa barua mwishoni mwa mwezi Mei ya kuwaomba
kurudia uchunguzi huo wa matiti.
Mamlaka ya
huduma ya afya -NHS imekadiri uchunguzi huo huokoa maisha ya mtu mmoja kati ya
200 ambao wamefanyiwa uchunguzi huo, na huyaokoa maisha ya watu 1,300 kwa mwaka
nchini Uingereza.
Lakini
kati ya wanawake 200 watatu ambao wamefanyiwa uchunguzi hupatikana na saratani
ambayo haihatarishi maisha ya binadamu na kujumuisha wanawake 4,000 kila mwaka
hupokea matibabu yasiyostahli.
Muuguzi
aliyestaafu Maggie Whyte , 61, kutoka Edinburgh aligundua kwamba alikuwa na
saratani ya matiti katika kiwango cha mwanzo alipokuwa ameenda kufanyiwa
uchunguzi wa mara kwa mara.
"Nilikuwa
na bahati ilikuwa haijasambaa kwenye tezi," alisema matibabu aliyoyapata
yalifanikiwa.
Uchunguzi
wa matiti hufanyiwa kila mwaka mara tatu kwa wanawake kati ya umri wa miaka
50-70 nchini Uingereza.
Taasisi ya
Madaktari wa Afya wa Uingereza (PHE) wamesema hawakuwa na habari zozote
kuhusiana na madhara ya uchunguzi huo hadi mwezi Januari.
Siku ya
Jumamosi, PHE ilisema itatoa usaidizi zaidi kwa wanawake ambao wamezidi umri wa
miaka 72 ili waweze kufahamu manufaa ya kufanyiwa uchunguzi katika siku zao
zijazo maishani.
Comments
Post a Comment