- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia kati benki yao na Kampuni ya Bima ya First Assurance kwa ajili ya kutoa Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kulia ni Bw. Bosco Bugali Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance.
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
UNITED Bank for Africa Tanzania(UBA) imetenga Sh.bilioni 23 ambazo zitatumika kukopesha wateja wa benki hiyo na wananchi ambao wanataka kukata bima kwa ajili ya usalama wa mali zao pindi yanapotokea majanga.
Hivyo ili kufanikisha wananchi wanapata huduma hiyo ya kukatiwa bima , UBA wameamua kushirikiana na Kampuni ya Bima ya First Assurance ya jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhakikisha wanaotoa bima kubwa za aina mbalimbali.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank for Africa Tanzania Ltd Usman Isiaka amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwawezesha wananchi wenye kuhitaji bima kuipata kwa kulipia kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mzima.
"Benki yetu itakachokuwa inafanya mteja anapokuja kwetu na kuelezea aina ya bima anayotaka kukata tunalipa fedha yote kwa kampuni ya bima ya First Assurance. Baada ya kutoa fedha hizo sisi tutakachofanya ni kumkata mteja fedha awamu kwa awamu kwa kipindi cha mwaka mmoja,"amesema.
Amefafanua benki yao pamoja na kutoa huduma mbalimbali za kibenki imeona haja ya kuwarahisishia wananchi katika kupata bima hiyo kwani ni muhimu katika usalama wa mali zao ila wanamini si wote wenye kuwa na fedha yote ambayo inahitajika kukata bima kwa wakati mmoja.
Amesema kwa watakaohitaji huduma hiyo wala hakutakuwa na dhamana yoyote zaidi ya kufuata taratibu ambazo wameziweka , hivyo wameomba wananchi kutumia fursa hiyo kwa kupata bima kwa kulipa kidogo kidogo.
Kwa upande wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya First Assurance Bosco Bugali amesema hatua ya benki hiyo kuamua kukopesha wanaohitaji kukata bima itatoa nafasi ya wananchi wengi kupata fursa ya kuwa na bima.
Amefafanua sheria inahitaji anayetaka bima kulipa fedha yote kwa wakati mmja, hivyo kitendo cha benki kutoa fedha na kisha mteja kurudisha kwa awamu itarahisisha.
Ameongeza kupitia benki hiyo sasa kila mwananchi atakuwa na uwezo wa kukata bima kubwa ambayo faida zake ni nyingi ukiilinganisha na bima ndogo hasa kwenye magari.
Bugali ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanakuwa na bima kwa ajili ya usalama wa mali zao na kusisitiza kipindi hiki cha kuelekea Serikali ya viwanda bima ina nafasi kubwa kwani kwa atakayekuwa na kiwanda akikata bima hana wasiwasi na mali zilizopo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance Bosco Bugali(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akielezea ushirikiano walioingia na benki ya United Bank For Africa (UBA) kwa ajili ya kutoa Bima ya Insurance Premium Financing (IPF) kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka
Afisa Mtendaji Mkuu wa First Assuarance Bosco Bugali na Mkurugenzi Mtendaji wa United Bank For Africa (UBA) Tanzania Ltd Bw. Usman Imam Isiaka wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa benki ya (UBA) na kampuni ya bima ya First Assurance mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari leo.
Comments
Post a Comment