- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MOSCOW, RUSSIA
Kuondoka kwa Senegal imeifanya Afrika kuandikisha matokeo
mabaya zaidi kwa miaka 36 tangu 1982- wakati Algeria na Cameroon waling'olewa
hatua ya makundi, Afrika iliwakilishwa kwenye hatua za mchujo kila mara. Lawama
kwa nani? bahati mbaya, VAR, au mipango dhaifu?
Kabla ya Urusi 2018, kulikuwa na matumaini Afrika
ingeendeleza maonyesho yake Brazil 2014 wakati wawakilishi wake wawili -
Nigeria na Algeria - walitua hatua za mchujo kwa mara ya kwanza.
Badala yake, bara zima litakuwa linajiuliza ni wapi chombo kilikwenda
mrama kwani timu za Afrika zimeandikisha ushindi mechi tatu na kufungwa 10
katika vipute vyao 15 kwa jumla.
Mfalme wa Misri Mo Salah kujeruhiwa.
Tunisia iliadhibiwa mechi zake za kwanza Kundi G kabla ya
kuifunga Panama waili hao wakifahamu kuelekea nyumbani. Ingawa Nigeria ilifunga
Iceland, pia imeondoka Urusi kwa kumaliza wa tatu Kundi D.Shindano hili
lilitarajiwa kuwa moja ambalo Misri ingebadili rekodi yake ya Kombe la Dunia
kwa kuwa na kikosi kizuri chenye mmoja wa wachezaji bora duniani.
Kwa mtazamo wowote ule, Mohamed Salah alitawala kampeni ya
kufuzu kwa Misri - kati ya mabao 10 ya Misri, Mo Salah alifunga saba na
kuchangia mengine mawili yaliyowasaidia kushiriki Urusi.
Aliyechukua nafasi ya Salah - Marwan Mohsen - mwenye goli
moja mechi 23 ya kimataifa - hakufanya lolote.
Hata iwapo Salah angekuwa hali nzuri ufanisi wa Misri
unazidi kutiliwa shaka baad aya kurejea jukwaa la Kombe la Dunia baada ya miaka
28 - walifanya makosa mengi kwenye ulinzi.
Mabeki Ali Gabr na Ahmed Hegazi hawakuelewana vyema licha ya
kunolewa na Hector Cuper - Kocha mwenye uzoefu idara ya Ulinzi.
Lakini wadakaji Mohamed El Shenawy na mkongwe Essam El
Hadary, 45, aliyeandikisha historia kwa kuwa Kipa mwenye umri wa juu zaidi -
walionyesha fomu nzuri katika mechi zao.
Hata hivyo, Misri haijatimiza mahitaji ya wengi kwani
kulikuwa na matarajio chungu nzima kwa mabingwa hao mara saba wa Kombe la
mataifa bora Afrika.
Simba wa Atlas wakosa
kung'ata
Kampeini ya Morocco ilionekana kuzimwa mwanzoni walipofungua
Kombe kwa kujifunga wenyewe dakika za mwisho dhidi ya Iran na kulazwa 1-0.
Kocha Herve Renard alitaja ngarambe hiyo "Fainali ya
Kombe la Dunia", kwa timu yake licha ya kusubiriwa na Ureno na Uhispania.
Uso wake baada ya mechi ulionyesha kuzidiwa na uchungu.
Kufuatia hapo, Morocco iliridhisha kwa pasi nzuri na
kuelewana.
Safu butu ya ufungaji iliwalemea kwani hawakuweza kuzitumia
nafasi zao mbele ya nyavu za wapinzani.
Mechi yao ya mwisho, Simba hao wa Atlas walikaribia kuilisha
Uhispania kichapo chake cha kwanza mechi 23 lakini mabingwa hao wa 2010
waliwalizimisha sare ya 2-2 dakika za mwisho kama ilivyo ada dhidi ya timu za
Afrika Kombe hili.
Morocco iliipa somo Uhispania licha ya kuwa na mastaa
wanaopiga Real Madrid na Barcelona, na baadhi yao kuichezea Manchester City,
Manchester United, Bayern Munich na Atletico Madrid.
"Ni timu bora sana iliyopoteza mechi mbili 1-0, na
ilistahili zaidi," alisema kocha wa Uhispania Fernando Hierro baadaye.
Nigeria - Timu ya siku
zijazo
Kufungwa dakika za mwisho na Argentina imeiumiza Nigeria na
kuvutia shtuma dhidi yake kutoka nyumbani, wengi wakistaajabu kwa nini ngome
yao haikupigwa jeki dakika za mwisho, lakini kampeini ya Super Eagles Urusi ni
ya matumaini bora siku za usoni. Ilikuwa na wachezaji 18 wenye umri mdogo
walioshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya Kwanza.
Licha ya kujumuishwa "Group of Death", walibakisha
tu dakika nne kufuzu hatua ya mchujo kabla ya bao la Marcos Rojo.
Nigeria ilikosa kuwasumbua wapinzani wake kipindi cha
kwanza.
Tofauti na makala ya awali ya Kombe la Dunia, Nigeria
haikukumbwa na sakata za malipo ya wachezaji, mambo hayo yalishughulikiwa miezi
kadhaa kabla ya Kombe la Dunia.
Tunisia bure
Tunisia haikuwa na nafasi ya kufuzu kutoka kundi ngumu lenye
Uingereza na Ubelgiji.
Tunisia iliadhibiwa mechi zake za kwanza Kundi G kabla ya
kuifunga Panama waili hao wakifahamu kuelekea nyumbani. Ingawa Nigeria ilifunga
Iceland, pia imeondoka Urusi kwa kumaliza wa tatu Kundi D.
Tunisia maarufu Carthage Eagles walilazwa na Uingereza dakika
za mwisho, Sawa na mataifa mengine ya Afrika, waliathirika kutokana na mabao ya
kuchelewa na mipira ya juu.
Ingawa kutokuwepo kwa nyota wao Youssef Msakni, imetajwa
kuwaumiza, mchango wake pia haungeweza kuwazuia walipobomolewa na Ubelgiji 5-2.
Mbali ya yote, Tunisia wameacha shindano wakiwa wafungaji
bora wa Afrika - mabao matano kutoka mechi tatu.
Mnamo 1978 walikuwa timu ya kwanza ya Afrika kushinda mechi
ya kwanza Kombe la Dunia.
Mhimili wa mwisho
waanguka
Senegal, iliyoonekana Kombe la Dunia tangu ilipofika robo
fainali 2002, ilisajili alama nne mechi mbili zake za kwanza Kundi H baada ya
kuifunga Poland na kutoka sare na Japan.
Imekuwa ni pigo kubwa kwa bara hili na ni kurudi nyuma hatua
moja kubwa kwani kuondoka kwa Senegal imeifanya Afrika kuandikisha matokeo
mabaya zaidi kwa miaka 36 amesema Drogba.
Senegal ni wa kwanza kuchujwa Kombe la Dunia kutumia sheria
za 'nidhamu' baada ya kulazwa na Colombia.
Simba hao wa Teranga walihitaji sare kufuzu wakichuana na
Colombia, na beki wake Kalidou Koulibaly alinukuliwa kabla ya mechi ugani
Samara akisema "bara zima lilikuwa nyuma ya Senegal".
Lakini mlinzi wa Colombia, Yerry Mina, aliitoa Senegal Kombe
la Dunia kwa kupiga kichwa hadi kimiani dakika ya 74 na kuwavunja moyo
mashabiki wa Senegal ugani Samara.
'Hatukustahili kufuzu'
"Hatujafuzu kwa kuwa hatukustahili kufuzu,"
alisema Aliou Cisse, kocha wa Senegal na kiungo mstaafu wa timu za Birmingham
City na Portsmouth.
"Pointi za nidhamu ni mojawapo za sheria na hizi sheria
zimewekwa kwenye mashindano kufuatwa. Tunafaa kuheshimu hilo.
"Tungechagua kutolewa kwa namna tofauti lakini ndiyo
inavyofanya kazi na tulijua ndio taratibu.
"Nimevunjika moyo, kwa kizazi hiki, na kwa wachezaji
hawa wanaolipigania taifa kila siku."
VAR iliifunga Afrika?
Mengi yanasemekana kuwa mtambo huo wa teknolojia Virtual
Assistant Referee (VAR) imewaumiza wengi.
Lakini Misri na Mohamed Salah walipata Penalti dhidi ya
Saudi Arabia kufuatia uamuzi wa VAR.
Hata hivyo, siyo Waafrika wote wameondoka Urusi.
Marefa kutoka Afrika wataliwakilisha bara hili kwa kusimamia
mechi zinazoendelea za hatua zilizosalia.
Comments
Post a Comment