- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka
mitatu na Ligi Kuu ya nchini Hipania (La Liga) kwa ajili ya kuendeleza mpira wa
miguu nchini Tanzania.
Hafla ya utiaji saini huo ilifanyika juzi, Juni 18, 2018 makao
makuu ya La Liga mjini Madrid, Hispania iliyohudhuliwa na Rais wa Laliga,
Javier Tebas, Mkurugenz wa Maendeleo ya Kimataifa wa La Liga, Oscar Mayo, mwakilishi
wa La Liga nchini Tanzania, Sami Hanane, Rais wa TFF Wallace Karia na Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura.
Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo, aliwaambia wanahabari
jana kwamba, hiyo ni hatua nyingine kwa La Liga kujikita kwenye mpira wa miguu
duniani na nia yake ya kushirikiana na taasisi mbalimbali za maeneo mbalimbali.
Ndimbo aliongeza kuwa, kupitia makubaliano hayo, La Liga
itaiongoza TFF katika mchakato wa kutengeneza Ligi inayojitegemea.
Pamoja na hayo, LaLiga kwa kushirikiana na TFF
watashirikiana kuandaa semina mbalimbali za ukocha, uongozi, uamuzi pamoja na
semina za maendeleo ya soka la vijana na wanawake.
Comments
Post a Comment