- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
LISBON, URENO
SANAMU ya awali ya mchezaji nyota wa Ureno na klabu ya Real
Madrid, Cristiano Ronaldo, ilipataa umaarufu sana duniani, lakini kwa sifa
ambazo walioiandaa hawakutarajia.
Ilizua mjadala kutokana na hali kwamba wengi wa mashabiki wa
nyota huyo waliamini haikuwa inafanana na Ronaldo.
Wengi hata walidhani ilimfanya aonekana mwenye tabasamu la
ajabu, au hata kama kibonzo.
Sanamu hiyo ilikuwa imewekwa kwenye kisiwa cha Madeira,
alikozaliwa CR7.
Iliwekwa kwenye uwanja wa ndege wa kisiwa hicho ambao pia
ulipewa jina lake baada ya Ureno kushinda Euro 2016.
Sasa, sanamu nyingine imewekwa na hiyo ya zamani kuondolewa.
Hii ya sasa inaonekana kidogo kukaribia kufanana na Ronaldo.
Lakini bado Cristiano hajasema anapendezwa na sanamu gani kati
ya hizo mbili.
Aliwika akicheza dhidi ya Hispania katika mchezo wa Kombe la
Dunia mwishoni mwa wiki ambapo aliwasaidia Ureno kutoka sare ya 3-3 kwa kufunga
mabao yote matatu ya taifa lake.
Comments
Post a Comment