- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya
kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bw,Nicomed Bohay akizungumza wakati wa kutambulisha fursa mpya kwa Wadau wa sekta ya Kilimo.
Baadhi ya Wadau wa Sekta ya Kilimo wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya PASS wakati wa utambulishaji wa fursa mpya kwa wadau wa sekta ya Kilimo.
Mwakilishi
wa AATIF, Bwana Samuel Ndonga akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam .
Meneja uwekezaji Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Mfuko wa UGEAP,Sonja Riedke akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya PASS.
Wadau wa sekt ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa taasisi ya PASS ,AATIF pamoja na Balozi wa Denmark nchi Tanzania ,Einar Jensen.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Binafsi ya
kusaidia sekta ya kilimo nchini (PASS) Bwana Nicomed Bohayakizungumza na Wanahabari muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Taasisi ya kusaidia sekta binafsi ya
kilimo nchini (PASS) imeingia makubaliano na Mfuko wa uwekezaji wa biashara na
kilimo Afrika (AATIF) kusaidia wadau wa sekta ya Kilimo nchini kwa kutoa mikopo
mikubwa itakayowezesha utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kilimo.
Makubaliano haya baina ya PASS na AATIF
yanatajwa kuwa mkombozi wa changamoto za muda mrefu za wadau wa sekta ya Kilimo ambao wamekuwa wakipitia
kwa kushindwa kupata mikopo ya muda mrefu kutoka kwa taasisi za kifedha hapa
nchini kutokana na ufinyu wa muda wa urejeshwaji wa mikopo hiyo.
Kwa kiasi kikubwa hali hii imekuwa
ikitajwa kama sababu ya sekta hii kushindwa kuwa na maendeleo makubwa kutokana
na mipango mingi kujikita katika uwekezaji wa muda mfupi.
Comments
Post a Comment