- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la watu na makampuni
yanayofanya biashara ya utalii kinyume cha sheria ikiwemo kutokuwa na Leseni ya
Biashara za Utalii (TTBL). Watu hao pia wamekua wakijihusisha na vitendo vya
utapeli na udanganyifu kwa watalii na hivyo kusababishia usumbufu mkubwa pamoja
kuharibu taswira ya sekta ya utalii na Taifa kwa ujumla.
Tunaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuweza
kuwabaini wote wanaohusika na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za
kisheria na iwe fundisho kwa wengine. Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008
Kifungu cha 10, 21 na 31(1-6) inamtaka mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii
kusajili na kulipa Ada ya Leseni ya Biashara ya Utalii kwa mwaka husika.
Tunasisitiza umma, watalii na wadau wa utalii kwa
ujumla kufanya biashara na kampuni zilizosajiliwa na Mkurugenzi wa Utalii na
kupewa leseni na Bodi ya Leseni ya Biashara za Utalii kuepuka kutapeliwa na usumbufu
mwingine utakaoweza kujitokeza.
Aidha, wafanyabiashara wa utalii, wapya na wale
wanaoendelea na biashara, wanajulishwa kuwa maombi ya usajili na utoaji wa
leseni za biashara za utalii kwa mwaka 2018 yanaendelea kupokelewa. Ni kosa
kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa
leseni.
Orodha ya wakala wa biashara ya utalii
waliosajiliwa na wenye leseni ya kufanya biashara ya utalii mwaka 2018 inapatikana
kwenye tovuti yetu ya Wizara, www.mnrt.go.tz
katika kipengele cha wadau (Stakeholders – Tour operators).
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya
Wizara, www.mnrt.go.tz au fika
katika ofisi zetu za Makao Makuu zilizopo Mtaa wa Kilimani, Barabara ya Askari
- Dodoma au Ofisi za Utalii za Kanda zilizopo Jengo la Mpingo - Dar es Salaam;
New Mwanza Hotel - Mwanza; Jengo la NSSF - Iringa na TANAPA Makao Makuu -
Arusha.
Maj. Gen. Gaudence Milanzi
KATIBU MKUU
21 Juni, 2018
Comments
Post a Comment