- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
KIGALI, RWANDA
MAMLAKA nchini Rwanda zimeuza mali ya familia ya mwanasiasa
aliye kizuizini ambaye pia ni mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame.
Diane Rwigara alizuiwa kuwania urais mwaka 2017 na baadaye
kakamatwa kwa madai ya udanganyifu na kuchochea mapinduzi ya serikali.
Halmashauri ya kukusanya ushuru nchini Rwanda iliuza mashine
kutoka kwa biashara ya familia ya tumbaku kwa takriban dola milioni 2 katika
hatua ya kulipia kodi, familia hiyo inaripotiwa kudaiwa zaidi ya dola milioni
7.
Familia hiyo inasema hatua hiyo ya kuuza mali na mashtaka dhidi
yake imechochewa kisiasa.
Mauzo ya awali ya biashara za familia ya Rwigara ya tumbaku
yalileta dola milioni 595.
Rwigara ni mtetezi maarufu wa haki za wanawake nchini Rwanda
na familia yake inasema matatizo yake yalianza wakati alipoamua kuwania urais.
Hakufaulu kuwania na alipigwa marufuku baada ya uchunguzi
kubaini kuwa Rwigara alikuwa amekiuka sheria kwa kukusanya sahihi bandia kuunga
mkono kugombea kwake.
Rigwara alikamatwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara Septemba
2017 nyumbani kwake kwenye mji mkuu Kigali.
Mama yake naye anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea
mapinduzi ya serikali.
Rais Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka 2017 kwa asilimia
98.63 ya kura.
Amesifiwa kwa kuleta mafanikio ya kiuchumi nchini humo tangu
yafanyike mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Comments
Post a Comment