- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
TEL AVIV, ISRAEL
ISRAEL imemuadhibu waziri wake wa zamani kwa kuipelelezea
Iran. Idara ya ulinzi wa ndani Shin Bet imesema.
Gonen Segev, daktari aliyewahi kuhudumu kama waziri wa
nishati miaka ya 1990, anadaiwa kusajiliwa na kampuni ya jinai ya Iran
alipokuwa akiishi Nigeria.
Alitiwa mbaroni alipozuru Equatorial Guinea mwezi Mei kabla
ya kusafirishwa kupitia ombi la polisi wa Israeli.
Segev mwenye umri wa miaka 62 alihukumiwa kifungo cha miaka
mitano mnamo 2005 kwa kosa la ulanguzi wa madawa na kuunda pasipoti feki ya
kidiplomasia.
Leseni yake ya kazi ilifutwa, lakini aliruhusiwa kufanya
kazi kama tabibu nchini Nigeria, alipohamia mwaka wa 2007.
Taarifa iliyotolewa na idara ya Shin Bet mapema leo ilisema
Segev alizuiliwa mwezi uliopita punde tu alipotua Israel.
Alichunguzwa kuhusu taarifa zilizodokeza kuwa huenda
alifanya mawasiliano na maajenti wa jinai wa Iran na kusaidia mikakati yao
dhidi ya Israel.
Wachunguzi walibaini kuwa Segev aliwasiliana na ubalozi wa
Iran nchini Nigeria mwaka wa 2012 na kuongeza kuwa alizuru Iran mara mbili
kukutana na wahusika wenzake, Shin Bet ilifafanua.
Imeongeza kuwa, Segev, alikutana na waajiri wake katika
mataifa mengine na alipewa mitambo ya kisasa ya mawasiliano kumwezesha kutuma
taarifa za kwa njia ya siri.
Shin Bet inadai kuwa Segev alitoa taarifa kuhusiana na sekta
ya nishati ya Israel, Maeneo ya usalama ya taifa hilo, na kuhusu maafisa katika
taasisi za kisiasa na usalama.
Aidha, Segev anadaiwa kuwaunganisha maafisa katika sekta ya
usalama ya Israel na waajiri wake aliowatambulisha kama waekezaji.
Siku ya Ijumaa, Segev alihukumiwa katika mahakama moja
Jerusalem kwa makosa ya "kumsaidia adui wakati wa vita na ujasusi dhidi ya
taifa la Israel", pamoja na makosa mbalimbali ya "kutoa taarifa kwa
adui".
Uamuzi wa kuzuia utoaji taarifa kuhusu kesi hiyo ilitolewa
Jumatatu lakini taarifa zaidi zimezuiwa.
Mawakili wa Segev wamesistiza kuwa hukumu hiyo imeonyesha
picha tofauti "Na kutofautiana na taarifa ya Shin Bett", Vyombo vya
habari vya Israeli vimeripoti.
Tangu vuguvugu la kiislamu la Iran kuanzishwa 1979, ambapo
viongozi wa kidini wenye misimamo mikali walipochukua hatamu, viongozi wa Iran
wameitisha kumalizwa kwa Israel. Iran inapinga haki ya kudumu kwa Israel,na
kuitambua kuwa mmiliki haramu wa ardhi ya waislamu.
Israel inaiona Iran kuwa tishio kwa kudumu kwake na imekuwa
ikisema kuwa Iran isiweze kupata silaha za kinuklia.
Viongozi wake wanahofia upanuzi wa Iran Mashariki ya Kati.
Comments
Post a Comment