Featured Post

DK. BILAL AKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUSOMA KURANI JIMBONI KIKWAJUNI

PIX%2B1
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akizungumza wakati wa Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wapili ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. 
PIX%2B2
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akimkabidhi zawadi, Salha Mohamed Khamis, baada ya kuibuka  mshindi wa juzuu tano wa  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni,Saleh Nassoro Jazeera  na  Mbunge wa Jimbo hilo, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kulia).
PIX%2B3a
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Salha Juma Sadalla akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika  leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.
PIX%2B3b
 Mshiriki wa Mashindano ya Kusoma Kurani, Abdilbaswit Hamis Hassan, akisoma kurani wakati wa mashindano yaliyofanyika leo katika Kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar. Picha na Mpiga Picha Wetu
PIX%2B4
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhandisi Hamad Masauni, baada ya kuwasili kiwanja cha Mapinduzi  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye  Mashindano  ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo visiwani Zanzibar.Wapili kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera. 
PIX%2B5
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal (watano kulia mstari wapili) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jimbo la Kikwajuni na washindi wa Mashindano ya Kusoma Kurani baada ya kuwakabidhi zawadi.Mashindano hayo yamefanyika katika Kiwanja cha Mapinduzi visiwani Zanzibar. 
PIX%2B6
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, akiwaaga wananchi (hawapo pichani), waliohudhuria  hafla ya  Mashindano ya Kusoma Kurani, yaliyofanyika leo  katika kiwanja cha Mapinduzi kilichopo Kikwajuni visiwani Zanzibar.Wakwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kulia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Saleh Nassoro Jazeera.

Comments