- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MOSCOW, RUSSIA
MSHAMBULIAJI wa Croatia, Nikola Kalinic, amefukuzwa katika
fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kukataa kuingia uwanjani wakati
wa mabadiliko ambapo Croatia ilishinda Nigeria 2-0.
Nafasi ya mchezaji huyo wa miaka 30 haitachukuliwa na mtu
mwingine ikimaanisha kuwa kikosi kitabaki na wachezaji 22 kwenye Kombe la Dunia.
Kalinic, mchezaji wa AC Milan, anasema ana jereha la mgongo
baada ya kulalamikia tatizo hilo wakati wa mechi ya kirafiki na Brazil.
Kocha Zlatko Dalic alisema: "Ninataka wachezaji wangu
wawe sawa na tayari kucheza."
Kalinic ambaye aliichezea Blackburn Rovers kati ya mwaka
2009 na 2011 amefunga mabao 15 katika mechi 41 alizoichezea Croata.
"Wakati wa mechi na Nigeria, Kalinic alikuwa akifanya
mazoezi na alistahili kucheza kipindi cha pili," Dalic alisema.
Lakini akasema kuwa, hakuwa tayari kutokana na matatizo ya
mgongo.
Croatia watacheza na Argentina siku ya Alhamisi na kumalizia
kundi lao la D dhidi ya Iceland Jumanne tarehe 26.
Wachezaji wengine watano waliohama Kombe la Dunia mapema:
Willie Johnston
(Scotland)
Mchezaji huyo wa West Brom alifukuzwa kutoka fainali za Kombe
la Dunia 1978 huko Argentina na Shirikisho la Kandanda la Scotland baada ya
kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu za mwili.
Roy Keane (Jamhuri ya
Ireland)
Kuondoka kwa kiungo huyo wa kati wa Manchester United kutoka
kambi ya mazoezi ya Jamhuri ya Ireland ilikuwa moja ya nyakati zinazokumbukwa
sana wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2002.
Hakufurahishwa na jinsi Ireland ilivyofanya maandalizi yake
hali iliyosababisha kuwepo majibizano na kocha Mick McCarthy mbele ya wachezaji
wengine.
Licha ya kujiandaa kucheza mechi ya ufunguzi na Cameroon,
Keane alibaki akitembea na mbwa wake kwenye mitaa ya Cheshire.
Diego Maradona
(Argentina)
Nyota huyo wa Argentina alitimuliwa kutoka kwa Kombe la Dunia
la mwaka 1994 nchini Marekani kabla ya mechi ya mwisho ya makundi na Bulgaria.
Alikuwa awali ameiongoza Argentina kwenda Kombe la Dunia la
mwaka 1986 alipoipatia taji na mwaka 1990 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani
kwenye fainali.
Maradona alifunga wakati wa ushindi wa mabao 4-0 kabla ya
kupatikana na kosa la kutumia madawa ya kuongeza nguvu za mwili na kufikisha
kikomo cha taaluma yake.
Nicolas Anelka
(Ufaransa)
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliondolewa kutoka kikosi cha taifa
nchini Afrika Kusini baada ya kutofautiana na kocha.
Mshambuliaji huyo ambaye wakati huo alikuwa akiichezea
Chelsea alimshambulia kwa maneno meneja wakati wa kipindi cha mapumziko wakati
wa mechi ya na Mexico mwaka 2010 walipofungwa mabao 2-0.
Alikataa kuomba msamaha na licha ya wachezaji wengine
kulamika jinsi alivyotendwa, aliamrishwa kurudi nyumbani na Shirikisho la Soka Ufaransa
na kupigwa marufuku ya mechi 18.
Zlatko Zahovic
(Slovenia)
Roy Keane hakuwa mchezaji pekee kuondoka Kombe la Dunia la
mwaka 2002 baada ya mchezaji wa Slovenia, Zahovic kumfuata nyuma.
Kiungo huyo wa Benfica wakati huo alikuwa na tofauti na
kocha Srecko Katanec baada ya kumuondoa uwanjani wakati wa mechi waliyofungwa
3-1 na Hispania ambapo shirikisho la kandanda liliamua kumtimua mapema.
Comments
Post a Comment