- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
ACCRA,
GHANA
Mwandishi
wa habari za uchunguzi Anas Aremeyaw Anas, kutoka nchini Ghana, amekataa
aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la Ghana, Kwasi Nyantakyi, kwamba mtu
fulani alimfuata na kumdai rushwa ya dola za Kimarekani 150,000 kwa lengo la
kuzuia uchapishwaji wa taarifa ya ripoti ya ubadhirifu wa fedha na rushwa.
Katika
taarifa ya utetezi wake binafsi, bosi huyo wa zamani wa GFA amedai kwamba
mwanasheria aliye karibu na Anas alimfuata na kudai kiwango hicho cha fedha ili
kufanikisha zoezi la kuzuia uchunguzi wa waraka huo.
Kama hiyo
haitoshi, Nyantakyi amedai kuwa, mwandishi huyo wa habari za uchunguzi na timu
yake walidukua barua pepe zake.
Lakini ameongeza
kudai pia kuwa kiasi cha fedha za Marekani dola 65,000 ambazo alionekana
akiziingiza kwenye mfuko katika mkanda uliorekodiwa kwa siri hazikuwa za ushawishi
bali dola 40,000 ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu kwa gharama za malazi
katika zoezi zima la jitihada za Morocco kutaka kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia
2026.
Katika
taarifa ya kukabiliana na Anas Aremeya Anas amekataa madai hayo akidai kwamba
bosi huyo wa zamani amepokea dola 65,000 kama rushwa, na kuongeza kuwa barua
pepe za bosi huyo hazikusitishwa kwa muda kumfikia na mtu yeyote wa upande
wake.
Wafanyakazi
wengi wa tasnia ya soka na viongozi walikamatwa kwa siri kwenye mkanda wa video
wakipokea zawadi za fedha inaarifiwa katika waraka wa uchunguzi na kuwaacha wa
Ghana walio wengi katika mshangao kutokana na hali hiyo.
Kwesi
Nyantakyi, baada ya madai hayo kuibuliwa amejiuzulu nafasi yake ya raisi wa
soka la GFA, mjumbe wa FIFA, Umoja wa Soka Afrika Magharibi na hata CAF.
Lakini
vita vya maneno baina ya Nyatakyi na Anas vinaendelea na huenda vikasababisha
mvutano mkubwa na mrefu sana kisheria.
Comments
Post a Comment