- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NA MWANDISHI WETU
BIASHARA ya Shirika la Ndege la Air Tanzania Company Limited
(ATCL) imepanda thamani kwa kipindi cha miaka miwili licha ya kuwa na abiria
wachache waliotumia ndege zake kusafiria.
Mkurugenzi wa biashara wa ATCL, Patrick Ndekana, aliambia
gazeti la Daily News kwamba biashara za shirika hilo la serikali
iliongezeka kutoka asilimia 2.5 mwaka 2016 hadi asilimia 42.6 mwisho wa mwaka
jana huku ikiwa na ndege mbili pekee zinazofanya kazi.
Amesema kuwa wana matumaini kwamba biashara hiyo itaimarika
zaidi baada ya kununuliwa kwa ndege mpya.
"Mwaka huu biashara yetu itaongezeka hususan baada ya
kuwasili kwa ndege ya tatu kubwa aina ya Bombadier Q-400s na baadaye kuwasili
kwa Bombadier nyengine mbili za Cs 300s ambazo zitakuwa na viti vingi,"
alisema.
Kwa sasa shirika hilo linamiliki ndege tatu aina ya Q-400
katika maeneo 10 tofauti nchini, mbali na kuelekea Comoro.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadi kufikia mwisho wa mwaka
jana, shirika hilo limekuwa likisafirisha abiria wachache na kufanya safari
chache ikilinganishwa na washindani wao.
ATCL inapanga kuleta ndege hizo mpya kupitia kuongeza safari
hususan katika maeneo ya Kaskazini, magharibi kaskazini mashariki.
Ndege hizo za serikali zinapanga kuanzisha safari za
kuelekea Bujumbura, Burundi kupitia Kigoma na Entebbe, Uganda kupitia
Kilimanjaro.
Ndekana amesema kuwa kufikia mwisho wa mwaka huu kampuni
hiyo itazindua safari nyengine za kuelekea Lusaka, Zambia na Harare, Zimbabwe.
"
"Safari hizo mpya za kuelekea Lusaka na Harare
zitaanzishwa mwezi Novemba, iwapo kila kitu kitafanyika kwa mpangilio,"
alisema.
Kampuni ya Boeing pamoja na shirika la ndege la Tanzania
zimethibitisha ununuzi wa ndege moja aina ya 787-8 Dreamliner, yenye thamani ya
Dola milioni 224.6.
Comments
Post a Comment