- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
KAMPALA, UGANDA
Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo
huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya
kijamii kama vile Facebook na WhatsApp.
Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata
Jumatano.
Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1
Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda
ambazo ni sawa na $0.05 ( £0.04) kila siku.
Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara
watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa
1% ya thamani yake.
Rais Yoweri Museveni alikaririwa na vyombo vya habari nchini
Uganda mwezi uliopita akisema kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa zaidi kwa
taarifa za "udaku".
Wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai ya
rais.
"Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa watu
kujieleza ," Mwana Blogi Rosebell kagumile aliliambia shirika la habari la
Reuters.
Takriban wabunge watatu wamekosoa sheria hizi mpya na
kuzitaja kama "utozaji wa kodi mara dufu ", kulinga na gazeti binafsi
Daily Monitor.
Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi,
almaarufu Bobi Wine - pamoja na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon -
wamesema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia
muda salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki.
Mbunge mwingine , Patrick Nsamba wa chama tawala , amesema
kuwa ushuru huo utawaumiza maskini zaidi.
Ni rahisi sana kwa mbunge kusema asilimia 1% ni kiasi kidogo
cha lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza
sana
Kuna mkanganyiko kuhusu namna ushuru huo mpya kwa mitandao
ya kijamii utakavyotekelezwa.
Waganda wanatumia mitandao ya kijamii kusambaza kauli zao za
kutoafikiana na ushuru huo mpya ambao umepitishwa kufuatia ombi la rais Yoweri
Museveni.
Katika barua yake kwa waziri wa fedha, Museveni alisisitiza
kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwa sababu inachochea taarifa za udaku.
Lakini alidai kuwa huduma ya data za intaneti haipaswi
kuwekewa ushuru, kwa sababu manufaa yake ya kielimu.
Serikali inahangai kuhakikisha simu kai zote zinasajiliwa.
Mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu ya kisiasa nchini
Uganda kwa chama tawala na upinzani.
Huduma ya mitandao hiyo ilifungwa wakati wa uchaguzi wa
2016.
Comments
Post a Comment