- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Eneo la Kitongoji cha Mferejini lililotengwa na Serikali kwa ajili ya kuanzisha kambi kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko.
Zaidi ya
watu wapatao 2000 wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya kufikwa mafuriko
kutokana na mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha huku eneo
lililoathirika zaidi na mvua hizo ni ukanda wa tambarare wa wilaya ya Same
unaopakana na Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Wahanga wa Mafuriko wakianza ujenzi wa nyumba za Miti kwa ajili ya kujisitiri katika eneo la Ruvu Mferejini.
Makazi ya wananchi hawa kwa sasa wanalala nje ,wakiteseka na Baridi,Mbu na wanyama wakali kama Nyoka hali ambayo inatishia Afya zao.
Hata hivyo tayari serikali imeanza kufikisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ya Maji kwa ajili ya kunywa pamoja na kupikia.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemery Senyamule akiwa ameongozana na Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour wakitembelea moja ya Kaya ya Jamii ya Wafugaji walioanza maisha mapya katika maeneo yaliyotengwa na Serikali.
Kama ilivyo ada kwa tamaduni za Mila za jamii ya Maasai kina mama ndio watendaji wakubwa wa shughuli za Nyumbani kiwemo ujenzi wa Nyumba kama anavyoonekana Bibi huyu.
Na hii ni Familia moja ya Fashet Kimotong wakiwa katika eneo jipya baada ya kuhama makazi yao ya wali kufuatiwa Nyumba zao kuzingirwa na maji .
Na Dixon
Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
SERIKALI
imetoa siku mbili kwa wananchi waliosalia katika Vijiji vya Ruvu Mferejini na
Ruvu Marwa wilayani Same ,Mkoani Kilimanjaro vilivyozingirwa na maji kuondoka
mara moja na kwamba watakao kaidi wataondolewa kwa kutumia nguvu na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria.
Licha ya
Idadi hiyo ya watu kuyahama makazi yao lakini bado wapo waliokaidi kuondokana na
hapa Serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Same ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Maafa ya Wilaya hiyo ,Rosemerry Senyamule ,ikatoa agizo.
Serikali
imetenga maeneo kando ya milima iliyopo katika kitongoji cha Mferejini kwa ajili
ya Kambi za Muda kwa watu waliokosa Makazi ,Clouds Habari imefika katika Kambi hizo
na kujionea maisha mapya ya wahanga wa mafuriko huku misaada ya kibinadamu
ikihitajika zaidi .
Licha ya
kukosekana kwa baadhi ya huduma katika eneo hili bado wananchi hawa wanahitaji
msaada wa hali na mali ili angalau kuweza kunusuru Maisha yao kutokana na
Baridi kali ,Mbu na hata wanyama wakali wakiwemo Nyoka.
Katibu
tawala mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi ,Aisha Amour ni miongoni mwa baadhi ya
viongozi waliowatembelea wahanga wa mafuriko kwa ajili ya kutoa pole .
Mafuriko
katika vijiji hivi yanatajwa kuwa hutokea kila baada ya Miaka 10 na kwamba mara
ya mwisho yalitokea mwaka 2008 huku chanzo kikitajwa kuwa ni kujaa kwa Bwawa la
Nyumba ya Mungu ambapo ujazo ulifikia Mita za ujazo 689.88 ambazo kwa sasa
zimeanza kupungua hadi kufikia mita za ujazo 689.80 baada ya maji kuanza
kuelekea kwenye maeneo ya makazi kwa kupitia mto Pangani.
Mwisho
Comments
Post a Comment