Featured Post

UJUMBE WA WIZARA YA NYUMBA NA MIUNDOMBINU NCHINI ZAMBIA WATEMBELEA SEKTA YA UJENZI

????????????????????????????????????
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Dkt. William Nshama, akizungumza na ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu pamoja na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia walipotembelea Wizarani hapo, mkoani Dodoma.

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu nchini Zambia,  Bw. Charles Mweshi, akiuliza swali kwa watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuhusu matumizi ya teknolojia stahiki ya nguvukazi katika kazi za ujenzi wa barabara, wakati walipotembelea wizarani hapo kwa ziara ya mafunzo, mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Dkt. William Mshama (hayupo pichani), wakati walipotembelea wizarani hapo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kazi za ujenzi wa barabara, mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Barabara kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Happiness Mgalula, akitoa uzoefu wa matumizi ya teknolojia stahiki ya nguvukazi katika kazi za ujenzi wa barabara kwa ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia, mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Meneja wa Kanda ya Kati kutoka Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi David Msekeni, akitoa mchango wa kitaalam kwenye  sekta ya ujenzi wa barabara kwa ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia, wakati walipotembela wizarani hapo kwa ziara ya mafunzo, mkoani Dodoma
????????????????????????????????????
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akisalimiana na ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia walipotembelea Wizarani hapo kwa ziara ya mafunzo, mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Sehemu ya wajumbe wa menejimenti ya Sekta ya Ujenzi, wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia walipotembelea Wizarani hapo, mkoani Dodoma.
????????????????????????????????????
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Dkt. William Mshama, akiagana na ujumbe kutoka Wizara ya Nyumba na Miundombinu na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC), nchini Zambia walipotembelea Wizarani hapo, mkoani Dodoma.

Comments