- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akihutubia washiriki wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula akihutubia washiriki wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) alikuwa mgeni rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza kuhusu fursa zilizopo Mkoani Dodoma wakati wa wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Dustan Kitandula akizungumzia manufaa ya kuanzishwa kwa Tume ya Madini wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki Kuzindua Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula wakati akimkabidhi vitendea kazi mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi vitendea kazi Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Shukrani Manya mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga ( kushoto) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Aderladus Kilangi( kulia) Wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya madini leo Jijini Dodoma.
Makamishana wa Tume hiyo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akimkabidhi Vitendea kazi mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Dkt. Florence Turuka ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Madini mara baada ya Kuzindua Tume hiyo leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Madini Mhe. Dotto Biteko (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Madini Mhe. Anjellah Kairuki wakati wa hafla ya kuzindua Tume hiyo iliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Anjelina Mabula akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Elias Kuandikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tume ya Madini leo Jijini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO , Dodoma
……………….
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Tume ya Madini imetakiwa kuhakikisha inatekeleza kikamilifu jukumu la usimamizi, Udhibiti, Ukaguzi, Ufuatiliaji, Ukusanyaji wa taarifa na kuweka kumbukumbu kwa kusimamia sekta hiyo kwa uadilifu hali itakayosaidia Taifa kunufaika na uwepo wa rasilimali madini.
Akizungumza wakati akizindua Tume hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kuzinduliwa kwa Tume hiyo kunaashiria kuanza kwa ukurasa mpya katika sekta ya madini nchini kwa kuwa uamuzi huo ni mapinduzi makubwa hali itakayosaidia wananchi kunufaika na sekta hiyo.
“Ni imani yangu, na pia ni imani ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na imani ya Watanzania wote kuwa mtatubadilishia simulizi za sekta ya madini kutoka kuwa za kukatisha tamaa na kuwa za matumaini, kuibadili historia ya sekta ya madini kutoka kuwa ya miguno na manunguniko na kuwa yakujivunia” Alisisitiza Mhe. Kairuki
Akifafanua Mhe. Kairuki amesema kuwa, si kwamba Tume hiyo imepewa mamlaka makubwa bali pia imepewa imani kubwa kwa kuwa mamlaka makubwa yanakuja na wajibu mkubwa mikononi mwa watendaji wa Tume hiyo.
Aliongeza kuwa Watanzania wana matarajio makubwa na Tume hiyo na viongozi wake kwa kuwa Serikali na wananchi wanaamini kuwa sekta hiyo sasa iko katika mikono safi na salama.
Kutokana na imani hiyo Mhe. Kairuki amesema kuwa wananchi wanaamini Tume hiyo itatenda haki, kusimamia ukweli na kuzingatia maslahi ya kizazi hiki na kijacho ili viweze kunufaika na madini ambayo Mwenyezi Mungu amelijalia Taifa letu.
Aidha, Mhe. Kairuki ameitaka Tume hiyo kuhakikisha inasimia kikamilifu wachimbaji wadogo kwa kuwatambua na kurasimisha shughuli zao ili sekta hiyo iwanufaishe kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kwa upande wa vibali vya mauzo ya madini nje ya Nchi amesema kuwa ni vyema Tume ikafanya mapitio ya fomu na vibali ili kuhakikisha kuna maelezo na taarifa za kina za madini yanayosafirishwa kuhusu yalipotoka (origin),.
Vile vile kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ameitaka Tume iandae mbinu na mikakati ya kudhibiti utoroshaji wa madini ili kudhibiti biashara haramu ya madini.
Tume ya madini imetakiwa kuangalia uwezekano wa kuweka utaratibu wa kutoa bei elekezi za madini ya aina mbalimbali ambapo utaratibu huo utawasaidia wachimbaji wadogo na wa kati.
Pia Mhe. Kairuki ameitaka Tume hiyo kuhakikisha kuwa kila anayefanya biashara ya madini ana leseni na ni leseni hai iliyolipiwa na kuhakikisha kwamba inathibiti watu au makampuni yanayomiliki leseni walizopewa kwa muda mrefu bila kuziendeleza kinyume na masharti ya leseni hizo.
Kuwepo kwa utaratibu wa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kuona maendeleo ya uwekezaji katika migodi ambayo imepata leseni ni moja ya jukumu ambalo Tume hiyo inatakiwa kulitekeleza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idrissa Kikula amesema kuwa wamepokea maelekezo yote ya Serikali na Tume hiyo iko tayari kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa .
Aliongeza kuwa Tume imejipanga kuhakikisha kuwa inatatua migogoro iliyopo katika sekta hiyo kwa kushirikisha vyama vyao vilivyopo katika maeneo yao.
Tume ya Madini imeundwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha kuwa rasilimali za Taifa zinawanufaisha wananchi wote, Kutokana na azma hiyo Tume imepewa jukumu la kusimamia sekta ya madini na Wizara ya Madini kubaki na Masuala ya kisera.
Comments
Post a Comment