- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI KATIKA MTAA WA KILIMAHEWA “A” KATA YA NYAMANORO WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHEDRACK MUGWE, MIAKA 30, MKAZI WA MKOLANI NA 2.JOAS SYLVELIUS MIAKA 24, MKAZI WA NYASAKA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA WAKIMILIKI KIWANDA BANDIA CHA KUTENGENEZEA POMBE BANDIA AINA YA BANANA WINE AMBAPO KATIKA ENEO LA TUKIO KULIPATIKANA CHUPA 400 ZENYE KIMIMINIKA BANDIA CHA PURE BANANA WINE ZIKIWA NA UJAZO WA MILILITA 330 KILA MOJA, MADUMU SABA YENYE UJAZO WA LITA 60 KILA MOJA ZA KIMIMINIKA BANDIA CHA BANANA WINE, STIKA 250 ZENYE NEMBO/CHAPA YA BANANA WINE NA PIPA MOJA TUPU LA PLASTIKI LA UJAZO WA LITA 60, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.
AWALI ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO NA DORIA WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU WAPO WATU WANAOMILIKI KIWANDA BANDIA CHA KUTENGENEZA POMBE BANDIA AINA YA BANANA WINE. ASKARI BAADA YA KUPOKEA TAARIFA HIZO WALIANZA KUFANYA UPLELEZI NA MSAKO KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU NDIPO BAADAE WALIFANIKIWA KUBAINI KIWANDA HICHO BANDIA NA KUWATIA NGUVUNI WATUHUMIWA HAO WAWILI TAJWA HAPO JUU PAMOJA NA VIELELEZO TAJWA HAPO JUU.
POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI, AIDHA UCHUNGUZI WA TUKIO HILI PIA UNAENDELEA KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI NYINGINE ZA SERIKALI AMBAZO NI TFDA NA TRA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATUHUMIWA WOTE WAWILI WATAFIKISHWA MAHAKAMANI, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA WAJIHUSHISHE NA BIASHARA HALALI ZA KUWAINGIZIA KIPATO NA WALA SI VINGINEVYO KWANI WASIPOFANYA HIVYO WATAANGUKIA KWENYE VYOMBO VYA DOLA NA BAADAE KUFUNGWA. PIA ANAENDELEA KUWASISITIZA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA BAADAE KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
Comments
Post a Comment