- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto), akimuonesha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baadhi ya vifaa tiba vinavyosambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), alipotembelea banda la MSD katika Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC). Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Mpoki Ulisubisya.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk.Mpoki Ulisubisya katika maonesho hayo.
Maonyesho yakiendelea.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiangalia bidhaa zinazosambazwa na MSD.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameipongeza MSD kwa kuteuliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo alipotembelea banda la MSD la maonyesho ambayo yanafanyika kando mwa Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika (Eastern, Central and Southern Africa Health Community, ECSA-HC).
Mkutano huo unajumuisha Mataifa tisa (9) wanachama ikiwemo Tanzania.
Comments
Post a Comment