- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
DAR ES SALAAM
27.3.2018
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani
Jafo amewasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Kigoma Ujiji
na Pangani Tanga kutokana na Ofisi zao kupata hati chafu katika Ripoti ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2016/17.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumanne (Machi 27, 2018), Waziri Jafo alisema Ofisi
yake imetekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais Dkt. John Pombe kuhusiana na
ripoti ya CAG kuwataja Watendaji hao kuzembea na kusababisha taasisi zao kupata
hati chafu.
Aliwataja
Wakurugenzi waliosimamishwa kazi na kupisha uchunguzi kuwa ni Bi. Hanji
Godigodi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Bw. Sabas Damian
Chambasi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
“Namwagiza
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI aunde timu ya Wataalamu kuchunguza utendaji
kazi wa Wakurugenzi hao na kunipatia taarifa ndani ya wiki tatu kuanzia leo”
alisema Waziri Jafo.
Kuhusu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma, Bw.
Judethadeus Mboya ambaye kustaafu utumishi, Waziri Jafo alisema uchunguzi dhidi
yake utaendelea kufanyika ili kubainisha kuhusika kwake katika kuisababishia
halmashauri hiyo kupata hati chafu.
Akifafanua
zaidi Waziri Jafo alisema katika taarifa hiyo ya CAG ya mwaka 2016/17, ripoti
hiyo ilibainisha kuwa katika ngazi za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuliwepo na
jumla ya vitabu 379 vya makusanyo ya mapato ambavyo havikuwasilishwa kwa CAG
kwa ajili ya kufanyika ukaguzi wa mahesabu yake.
Aliongeza
kuwa kutokana na taarifa hiyo, Ofisi yake itawasiliana na Wakurugenzi wote
kuhakikisha kuwa inawasilisha vitabu hivyo vyenye taarifa na nyaraka za ukaguzi
katika ofisi ya CAG haraka iwezekanavyo.
Kwa
mujibu wa Jafo alisema kwa sasa Serikali imepata mafanikio makubwa sana katika
suala zima la udhibiti wa matumizi ya fedha za Serikali katika mamlaka za
Serikali za Mitaa ikilinganisha na miaka ya nyuma ambao hali ya matumizi
haikuwa nzuri.
Waziri
Jafo alizipongeza Halmashauri 166 zilizopata hati safi na kuendelea kufanya
vizuri katika kusimamia taratibu za matumizi ya fedha za umma pamoja na
kuzitaka halmashauri 16 zilizopata hati isiyoridhisha kufanya maboresho katika
utendaji kazi ili kupata hati safi.
“Kwa
upande wa Halmashauri zilizopata hati chafu naziagiza zibadilishe mienendo ya
utendaji kazi katika halmashauri zao sambamba na kuyaagiza Mabaraza ya Madiwani
kusimamia vyema Halmashauri hizi katika mipango ya matumizi ya fedha za
Serikali” alisema Jafo.
Comments
Post a Comment