- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka baina ya Tanzania na Kenya kilichoharibika
eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua
mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula akiangalia alama ya kimataifa katika mpaka baina ya Tanzania na
Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya
kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula akiangalia kigingi cha mpaka baina ya
Tanzania na Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa
ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga wakiangalia eneo la
mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la
Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka
wa Tanzania na Kenya
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula akiangalia eneo la mpaka baina ya Tanzania na Kenya katika eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa
mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula akiangalia eneo la mpaka baina ya Tanzania na Kenya katika eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime mkoa wa
mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Angelina Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga wakiwa katika picha
ya pamoja na Askari wa Kenya wa hifadhi ya Masai Mara ambayo inapakana na
hifadhi ya Serengeti wakati alipokagua mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.
Gari ya doria ya askari wa hifadhi ya Masai
Mara ya nchini Kenya ambayo imepakana na hifadhi ya Serengeti ikiwa katika msafara wa Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati wa kukagua mpaka wa
Tanzania na Kenya uliopo ndani ya hifadhi ya Serengeti.
Mto Mara uliopo katika hifadhi ya Serengeti Wilaya
ya Tarime Mkoa wa Mara.
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI- WANMM)
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula amesema Serikali
itaanza kuweka alama za mipaka ya kimataifa katika mipaka yake na nchi jirani za
Kenya na Uganda kuanzia machi mwaka huu.
Hatua
hiyo inafuatia baadhi ya alama za mipaka yake na nchi jirani katika maeneo
mbalimbali kuharibika ama kuchezewa na
hivyo kuleta mkanganyiko baina ya Tanzania
na nchi hizo ni wapi mwisho wa mipaka.
Akizungumza
katika ziara yake mkoani Mara, Mabula amesema kwa sasa fedha kwa ajili ya kazi
hiyo imeshatengwa na kinachosubiriwa ni kuanza rasmi kwa kazi hiyo hapo machi
mwaka 2018.
‘’katika
zoezi la kuweka alama za mipaka vitawekwa vigingi kila baada ya umbali wa mita
mia moja sambamba na kubainishwa eneo la ardhi huru’’ alisema Mabula.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi, tayari timu ya
wataalamu kutoka nchi za Kenya Uganda na Tanzania zimeshakutana na kukubaliana kuhusiana
zoezi la uainishaji mipaka ya nchi hizo.
Aidha,
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kwa sasa alama zitawekwa katika
mipaka iliyopo mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga na baadaye zoezi
litaendelea katika maeneo mengine ya mipaka.
Amesema,
ni imani yake baada ya kukamilika kwa zoezi la kuweka alama za kimataifa za
mipaka suala la migogoro kuhusiana na mipaka litakwisha.
Kwa
mara ya mwisho zoezi la kuweka alama za mipaka ya kimataifa baina ya Tanzania
na nchi jirani lilifanyika mwaka 1975 baada ya lile la awali la Tangazo la
Serikali (GN) mwaka 1965 kuhusiana na mipaka.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Grorious Luoga alimueleza naibu waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kuwa, mbali na suala la mipaka ya kimataifa wilaya yake
inakabiliwa na changamoto ya mipaka baina ya hifadhi ya Serengeti na wananchi
wanaozunguka hifadhi hiyo kwani wamekuwa wakivamia na kujenga ndani ya hifadhi
na wakati mwingine kuingiza mifugo.
Katika
ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya katika eneo la Serengeti,
Naibu Waziri wa Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi Mabula alifuatana na Mkuu
wa Wikaya ya Tarime Glorious Luoga pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Upimaji Vijijini
kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Huruma Lugalla ambapo kwa
pamoja walijionea hali halisi ya mpaka wa Tanzania na Kenya na baadhi
ya alama za mipaka zilizoharibika.
Comments
Post a Comment