- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina mabula akitafuta kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kwa kuchimba eneo ambalo kigingi hicho kilikuwepo katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Horohoro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akipita katika kichaka kuelekea katika kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa nchi hizo mbili eneo la Horohoro.
Na Mwandishi Maalum,
Mkinga Tanga
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amebaini uwepo ya
nyumba za watanzania zilizojengwa katikati ya mpaka wa Tanzania na Kenya huku
eneo moja la nyumba hizo likiwa upande wa Kenya.
Katika
ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo la Horohoro mkoa wa
Tanga mhe Mabula alijionea jinsi nyumba zilivyojengwa bila utaratibu wa kuacha
umbali wa mita mia kama eneo huru.
Eneo
lililoathirika zaidi na ujenzi huo, ni katika kitongoji cha Jasini kijiji cha
Mahandakini wilaya ya Mkinga ambapo asilimia kubwa ya wakazi wake wamejenga
nyumba zao zikiwa karibu kabisa na mpaka huku baadhi yake sehemu ikiwa upande
wa Tanzania na nyingine upande wa Kenya.
Hata
hivyo, Naibu Wzairi wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameshuhudia upande
wa Tanzania katika eneo la Horohoro ukiwa umezingatia umbali unaotakiwa kati ya
mpaka ukilinganisha na wakenya wanaoishi kijiji cha Jua kali Lungalunga ambao
wamejenga karibu kabisa na mpaka wa Tanzania.
Kufuatia
hali hiyo kuna uwezekano mkubwa wakazi wanaoishi katika maeneo hayo ya mpakani
kukumbwa na zoezi la kubomolewa nyumba zao ingawa kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea baina
ya Tanzania na Kenya kuhusu umbali gani pande hizo zinaweza kukubaliana ili
kunusuru baadhi ya wananchi wa pande zote mbili.
Akizungumza
katika ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya, Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amesema, kwa sasa umbali
unaotambulika kama eneo huru baina ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja ingawa
kuna mazungumzo yanayoendelea katika ngazi ya wataalamu juu suala la umbali wa
eneo huru.
Kwa
mujibu wa Mabula, pamoja na sheria kuweka bayana kuwa umbali unaotakiwa katika
eneo huru kati ya Tanzania na Kenya ni mita mia moja lakini pande hizo zinaweza
kukubaliana kama ilivyofanyika kwa nchi ya Uganda na Burundi ambapo kwa Uganda
eneo huru litakuwa mita thelathini huku Burundi likiwa mita kumi na mbili na
nusu.
Amesema,
ukaguzi wa mipaka anaoufanya una lengo la kuhakikisha mipaka ya Tanzania na
nchi jirani inakuwa katika hali nzuri hasa ikizingatiwa alama za mipaka
zilizopo ni za muda mrefu huku baadhi yake zikiwa zimeharibika.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesisitiza kuwa, kwa sasa
Tanzania haina mgogoro na Kenya juu ya mipaka na kinachofanyika ni kuimarisha
usalama wa nchi zote mbili hasa ikizingatiwa njia za panya ziko nyingi.
Mabula
amesema, awamu ya kwanza ya kuweka alama za mipakani itafanyika katika mipaka
baina ya Tanzania na Kenya pamoja na mpaka kati ya Tanzania na Uganda na fedha yote
kwa ajili ya kazi hiyo imeshatolewa kinachosiriwa ni kuanza tu kwa zoezi..
Mkuu
wa wilaya ya Mkinga Yona Maki alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mabula kuwa Wilaya yake imekuwa lango la raia wanaokimblia
afrika kusini, dawa za kulevya kama mirungi na mpango wa wilaya ni kutaka
kufyeka miti na vichaka vilivyopo katika mpaka kati ya Tanzania na Kenya.
Aidha,
amesema wilaya ya Mkinga ina tatizo la wahamiaji waloweza na zoezi la
kuwatambua limeanza ili kuwabaini
sambamba na kuthibiti vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula amehitimisha
ziara yake ya siku kumi na mbili mkoa wa Tanga, ziara iliyokuwa na lengo la
kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi pamoja na uhamasishaji ulipaji kodi hiyo ambapo ziara ilianzia mkoa Mara, Arusha na
Kilimanjaro.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia
kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya katika kitongoji cha Jasini kijiji
cha Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga. Nyuma zinazoonekana nyumba zimejengwa
katikati ya mpaka huo wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka baina ya Tanzania
na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiangalia baadhi
ya nyumba zilizojengwa katika mpaka wa Tanzania na Kenya katika kijiji cha
Mahandakini wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga wakati wa ziara yake ya kukagua
mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula (wa nne
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Mkinga mbele ya
nyumba iliyojengwa upande ukiwa Tanzania na mwingine Kenya, kuanzia diwani
Hassan Bakari Ally (wa nne kulia aliyevaa kofia) kuelekea kulia wako upande wa
Kenya.wengine ni Mkuu wa wilaya ya Mkinga Yona Maki (wa pili kulia) na wa tatu
kushoto ni mbunge wa jimbo la Mkinga Dustan Kitandula.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akioneshwa
kigingi cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya kilichowekwa wakati wa utawala wa
muingereza na Mwenyekiti wa kijiji cha Mahandakini wilaya ya Mkinga Nassoro
Mbarouk Nassoro wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina mabula akieleza
jambo mara baada ya kupata maelezo juu ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha
Saruji, nishati ya umeme joto, mabegi, vifaa vya ujenzi pamoja na bandari ndogo
katika eneo la Mtimbwani wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga kutoka kwa mkuu wa
wilaya ya Mkinga Yona Maki wakati alipofanya ziara ya kukagua mpaka wa Tanzania
na Kenya.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akipata
maelezo kuhusiana na mpaka wa Tanzania na Kenya kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji
cha Mahandakini Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga Nassoro Mbarouk Nassoro wakati
wa ziara yake ya kukagua mpaka wa Tanzania na Kenya.
Naibu
waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa katika
picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Mkinga mkoa wa Tanga mara
baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua mpaka kati ya Tanzania na Kenya eneo
la Horohoro. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Yona Maki na wa nne
kulia ni Mbunge wa jimbo la Mkinga Danstan Kitandula. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya
Comments
Post a Comment