Featured Post

NAIBU KATIBU MKUU UWT EVA KIHWELE AMEVUNA WANACHAMA WAPYA ZAIDI 300 KATIKA TARAFA YA MAZOMBE MKOANI IRINGA

Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiongea na wananchi pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa.
 
Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele akiwapatia kadi wanachama wapya wa umoja wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa

 Naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja na wanachama wa chama cha mapinduzi Tarafa ya mazombe wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa akiwa sambamba na viongozi wa umoja huo mkoani Iringa wakiwasindikiza wanachama wapya kula kiapo cha kukitumikia chama hicho
 Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwaonge na wananchi pamoja na wanachama wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa.

 Na Fredy Mgunda, Iringa
NAIBU katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele amevuna wanachama wapya zaidi ya mia tatu (300) katika tarafa ya Mazombe wilayani Kilolo mkoani Iringa ambo wamejiunga rasmi na umoja huo.

Wanachama hao wamepokelewa wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, ambapo naibu katibu mkuu bara Eva Kihwele alipokuwa akiongea na wanachama pamoja na wananchi wa tarafa ya Mazombe ndipo waliposhawishika kujiunga na umoja huo kutokana na hamasa walioipata kutoka kwa katibu huyo.

Kihwele alisema kuwa chama cha mapinduzi ni chama ambacho kimejengwa kimisingi ya kulea jumuhia  mbalimbali ambazo zipo ndani ya chama hicho ndio maana bado kinanguvu katika siasa za hapa nchini hata kimekuwa mfano kwa nchi nyingine.

“Jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi Tanzania ni moja kati ya jumuiya ambayo ipo ndani ya chama hiki na inakazi zake kwa ajili ya kukijenga chama na kuleta maendeleo kwa wananchi waliokipa dhamana ya kuongoza nchi hii” alisema Kihwele


Aidha Kihwele aliwataka wanawake kujifunza kujifunza kujitegemea ili waweze kuja kuwaajiri wanaume ambao kwa sasa ndio wamekuwa wakitoa ajira nyingi kwa wanawake hapa nchini.

“Wanawake wenzangu sasa imefika mwisho wa kuwa tegemezi kwa wanaume inatakiwa sasa tusimame sisi kama sisi na tuanze kuwaajiri na kulisha wanaume zenu majumbani kwetu maana tunauwezo wa kufanya kila kazi hizo inatakiwa tujitume” alisema Kihwele

Kihwele alisema kuwa wanawake mkiwa mnataka kufanya biashara zenye malengo msiogope kwenda kukopa maana siku hizi kuna mikopo ya bei rahisi na riba yake sio kubwa ambayo itakuwezesha kufanya biashara yako kwa maendeleo yako.

“Siku hizi kuna mabenk mengi yanawakopesha wanawake na wanawaamini sana wanawake kwenye kufanya biasha hivyo nendeni mkakope msiogope maana hizi benk zipo kwa ajiri ya kusaidia kuinua maisha ya mtanzania” alisema Kihwele

Kihwele alimalizia kwa kuwataka wanawake wa kata ya Mkwawa mkoani Iringa kuzitumia pesa kwa nidhamu ya hali ya juu ili ziweze kuleta matunda ya kuleta maendeleo ambayo yanahitajika kwa maisha yao.

“Jamani kila pesa ukiitumia kwa nidhamu basi utaona faida yake na itakuletea maendeleo yako na taifa kwa ujumla maana unakuwa umetumia vizuri pesa kwa maendeleo” alisema Kihwele

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve alisema kuwa atawapatia elimu ya ujasiliamali ili wakipata mitaji waweze kuitumia vizuri kwa ajili ya manufaa ya maendeleo.

“Jamani mimi nimekuwa nikitoa elimu ya ujasiliamali mara kwa mara kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufanya biashara zenu kwa faida na kutoa elimu ya matumizi ya fedha hivyo nawaomba nikiitisha tena kutoa elimu mkaribia kwa wingi maana huwa inakuwa bure” alisema Twelve

Naye Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer amewataka wanawake kote nchini kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za ujasiriliamali ili kuachana na utegemezi.

Laizer alisema kuwa baadhi ya wanawake hasa wa vijiji wamekuwa wakipata msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kipato licha ya kushiriki shuhuli za uzalishaji mali ngazi ya familia lakini wengi wao wamekuwa hawashirikishwi katika matumizi ya kipato walichokitolea jasho. 

Laizer alisema kuwa kuna mifuko maalumu ya kuwaisidia wanawake hasa wa hali ya chini kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi ili kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuachana na utegemezi hivyo msaada walioupata utawafanya wapige hatua kubwa zaidi.

Laizer alisema kuwa kumsaidia mwanamke wa hali ya chini kwa kumuwezesha kimtaji ni kukomboa jamii kwani mama huyo ataweza kuhuduma familia yake bila ya kuwa tegemezi.

Comments