- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Hali Ya Uchumi - Press 28 Desemba 2017 by Maendeleo Vijijini on Scribd
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Susana Mkapa na Afisa Mwandamizi wa Wizara hiyo Bw. John Sausi wakizungumza jambo wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na Waandishi wa Habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakifurahia jambo wakati Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo aliangazia suala la hali ya Uchumi na kubainisha kuwa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaabani (kushoto) akizungumza na wadau waliohudhuria Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na waandishi wa habari katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kulia.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Hali ya uchumi na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 ambapo alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kuwakamata wanaowalazimisha watanzania kufanya malipo kwa Dola badala ya Shilingi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb) (mbele) akiwa katika Mkutano na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi
na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2017/18 katika ukumbi wa Wizara
ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha
na Mipango)
Comments
Post a Comment