Featured Post

WANANCHI JIJINI DAR ES SALAAM WAIPONGEZA KAMPUNI YA ABACUS PHARMA (A) LTD

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu (kulia), Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga  na Dk. Mohamed Mohamed wa ugonjwa wa Kisukari katika hospitali hiyo wakikata keki maalumu iliyotengenezwa kwa bidhaa za Sugar Free zisizo na sukari wakati wa uzinduzi  wa bidhaa hizo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

 Muonekano wa keki hiyo iliyotengenezwa kwa bidhaa hizo zisizo na sukari.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu, akizungumza bidhaa hizo. (Kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa hizo piga simu namba 0784834010)
Hii ndiyo timu ya maofisa masoko wa kampuni hiyo.

Na Dotto Mwaibale
WANANCHI jijini Dar es Salaam na vitongoji vyake wameipongeza  Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD kwa kuwaletea bidhaa za Sugar Free ambazo zinasaidia kupunguza  matumizi makubwa ya sukari kwenye vyakula.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam walisema kampuni hiyo haina budi kupongezwa kwa kuzileta bidhaa hizo katika soko la Tanzania ili kukabiliana na changamoto ya matumizi kupitia vyakula.

"Hivi sasa kila pembe ya nchi yetu kumekuwa na changamoto ya ugonjwa wa kisukari ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mfumo wa ulaji na unywaji wa vyakula vyenye sukari kupita kiasi kwa bidhaa hizi mpya zinazosambazwa na Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD hakika itasaidia sana" alisema Frank Erasto mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam.

Erasto alisema yeye ni mihongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa kisukari lakini tangu bidhaa hizo ziingie katika soko la Tanzania amekuwa akitumia bidhaa hizo ili asiongeze sukari mwilini mwake baada ya kupata matibabu.

Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina moaja la Reuben alisema familia yake imeanza kutumia bidhaa hizo ambazo hazina gharama kubwa.

"Familia yangu na marafiki zangu tumeanza kutumia bidhaa hizi za Sugar Free kusema kweli ni nzuri na zina radha kama ile zilizopo kwenye chakula halisi" alisema Reuben.


Mkazi wa Kariakoo Happyness Kimaro alisema kwake anaona bidhaa hizo ni mkombozi kwani ameanza kuzitumia baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa kisukari na hapendi kuongeza sukari mwilini mwake.

"Sisi wagonjwa wa kisukari tumekuwa na changamoto kubwa ya ulaji wa vyakula mara tunaambiwa tusile hiki na kile tule vyakula ambavyo havina sukari ambavyo havina ladha sasa kwa kuletewa bidhaa hizi tunasema ni nafuu kwetu" alisema Kimaro.

Akizungumza bidhaa hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Abacus Pharma (A) LTD, Ramesh Babu alisema bidhaa hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matumizi makubwa ya sukari katika vyakula. 


Alisema bidhaa hizo zimetengenezwa mahususi ili kukabiliana na ongezeko la sukari mwilini na hivi sasa zinapatikana kwa bei ya chini katika soko la nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi na kuwa bei hizo zipo kuanzia shilingi,4200, 4,500, 5,700, 8,850 na za bei ya juu ni shilingi 13,000 na kuwa zinategemea bidhaa husika.

"Bidhaa hizi zipo za aina mbili za sugar free gold  ambazo hutumika katika chai, uji, na vinywaji baridi tu  na sugar free natura hutumika katika baking, kupikia vyakula vinavyohitaji sukari katika upishi na pia hutumika katika chai, uji na vinywaji baridi na matumizi yake ni rahisi sana," alisema Babu.

Alisema kwa Tanzania bidhaa hizo zimeanza kuchukua soko kubwa baada ya wananchi kuona umuhimu wake na hivyo wanategemea muitikio utaendelea kuwa mkubwa.

Aliongeza kuwa, lengo kubwa la kampuni hiyo kusambaza bidhaa hizo ni kusaidia jamii kuelewa matumizi ya bidhaa hizo ambazo hazina sukari ingawa zina ladha ya sukari kama ile ya kawaida  na kwamba bidhaa hizo zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).


Akizungumza katika uzinduzi wa bidhaa hizo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya homoni na Kisukari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Faraja Chiwanga alisema ugonjwa wa kisukari ni changamoto kubwa kwani Tanzania ni nchi ya tano Barani Afrika kwa kuwa na wagonjwa wengi.


Alisema hali hiyo inatokana na watu wengi hasa vijijini kutojijua mapema kama wameathiriwa na ugonjwa huo ambapo baadhi yao huanza kugundua baada ya kupata upofu, kukatwa miguu na kadhalika. 


Aliongeza kuwa, matibabu ya mgonjwa mmoja wa kisukari yanafikia asilimia 25 ya pato la familia fedha ambazo ni nyingi jambo linalowafanya wauguzaji kukata tamaa ya kumtibu mgonjwa na kuamua fedha hizo kuzielekeza katika matumizi mengine.


Dk.Chiwanga alitoa mwito kwa kusema ni vizuri kuzuia kupata kisukari kuliko kutibu.

Akizungumzia bidhaa za sugar free alisema hazitibu ugonjwa wa kisukari isipo kuwa zinamsaidia mgonjwa au mtu mwenye kisukari anapokula vyakula vingine visivyo na sukari kupata radha ile ile.

Alisema mtu mwenye ugonjwa wa kisukari hatakiwi kabisa kuvuta sigara ingawa vitu vingine kama vinywaji na pombe anatakiwa kutumia kwa uangalifu.

Comments