- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA
MIPANGO
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU
MATUMIZI YA FEDHA ZA KIGENI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maagizo kuhusu matumizi ya fedha
za kigeni katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kusisitiza kuwa utekelezaji wake uanze tarehe 1 Januari, 2018. Maagizo hayo ni kama ifuatavyo: -
i.
Bei zote hapa nchini zitangazwe kwa shilingi ya
Tanzania. Bei hizi zinajumuisha kodi ya nyumba za kuishi na maofisi, bei ya
ardhi, gharama za elimu na afya, bei za vyombo vya usafiri na vifaa vya
kielektroniki.
ii.
Bei ambazo walengwa wake wakuu ni watalii au wateja
wasio wakazi zinaweza kutangazwa kwa fedha za kigeni na malipo yake yanaweza
kufanyika kwa fedha za kigeni. Bei hizi zinajumuisha gharama za usafirishaji
kwenda nchi za nje kupitia Tanzania, gharama za mizigo bandarini kwenda nchi za
nje, gharama za viwanja vya ndege na viza kwa wageni, na gharama za hoteli kwa
watalii kutoka nje ya nchi. Walipaji wanaotumia fedha za kigeni watambuliwe kwa
vitambulisho vyao kama pasi za kusafiria na nyaraka za usajili kwa makampuni.
iii.
Viwango vya kubadilishana fedha vitakavyotumika
katika kuweka hizo bei katika sarafu mbili viwekwe wazi na visizidi vile vya
soko. Ifahamike wazi kuwa ni mabenki na maduka ya fedha za kigeni tu
yanayoruhusiwa kupanga viwango vya kubadilisha fedha kutokana na ushindani
katika soko la fedha za kigeni.
iv.
Mkazi yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia
bidhaa au huduma yeyote hapa nchini kwa fedha za kigeni.
Aidha Dkt. Mpango ameviagiza vyombo vya dola
viwachukulie hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo haya ya
Serikali.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Comments
Post a Comment