- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS MAGUFULI AWASILISHA FOMU ZAKE ZA TAMKO LA RASILIMALI NA MADENI KWA VIONGOZI WA UMMA KATIKA OFISI ZA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari
House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa ajili
ya kuwasilisha Fomu zake za Tamko la
Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa
Maadili, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold
Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika
Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo
katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa
Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold
Nsekela mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni
kwa Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya
kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma
katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwepo
katika jengo la Sukari House wakati akitoka katika katika Ofisi za Sekretarieti
ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa
Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold
Nsekela wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti
ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika jengo la
Sukari House jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi
walio simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika
Ofisi za za Sekretarieti ya Maadili ya
viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment