- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi Mhe. Dkt Mwigulu L.Nchemba akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Mhe. Christina Mndeme na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa Ndugu Andrew W. Massawe wakiwasili kwenye viwanja vya Lisaboni –Songea
kushiriki sherehe za uzinduzi wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoa
wa Ruvuma.
Mhe.Dkt Mwigulu L.Nchemba akikagua
baadhi ya Vitambulisho 3470 ambavyo
watagawiwa wananchi wa Kata ya Songea ambao Usajili wao umekamilika kufuatia
zoezi la Usajili Vitambulisho kuwa kufanyika katika Kata za karibu kabla ya
kuanza Usajili wa Umma. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme
na Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida Ndugu Andrew W. Massawe.
Mhe Waziri akimkabidhi
Kitambulisho chake mmoja wa wananchi wa Kata ya Songea Bwana Hassan Ally
Shomari wakati wa zoezi la ugawaji Vitambulisho kwenye sherehe za uzinduzi wa
zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma. Jumla ya Vitambulisho 3470 viligawanywa
kwa wanachi wakati wa sherehe hizo.
Kikundi cha burudani za
asili maarufu kama wana Lizombe wakitumbuiza wakati wa sherehe za uzinduzi wa
zoezi la Usajili kwa mkoa wa Ruvuma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho
vya Taifa (NIDA) Ndg Andrew W. Massawe ameitaja mikoa ya Mara, Arusha, Iringa,
Geita, Lindi, Simiyu, Mbeya na Songwe kuwa mikoa
inayoongoza katika zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa;
huku mikoa mingine ikiwa nyuma kiusajili kulinganisha na malengo waliyowekewa.
Akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa zoezi la
usajili kwa mkoa wa Ruvuma lilofanyika katika viwanja vya Lisaboni-Songea,
Ndugu Massawe amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba
kusaidia kuweka msukumo kwa viongozi na wananchi kwenye mikoa ambayo haifanyi
vizuri ili iongeze kasi ya usajili kwa lengo la kukamilisha usajili kwenye mikoa
yao kwa muda uliopangwa.
Akihutubia wananchi wa Ruvuma waliofurika kwenye
viwanja vya Lisaboni vilivyopo nje kidogo ya mji wa Songea, Waziri wa Mambo wa
Ndani ya Nchi Mhe.Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amewasisitizia wananchi kujitokeza
kwa wingi kusajiliwa kwani kuwa na kitambulisho cha Taifa siyo suala la hiyari
ni wajibu kwa kila Mtanzania mwenye sifa kuwa nacho.
“ Mhe. Rais wetu ametoa hela za kuwasajili, zoezi
ni bure bado kujisajiliwa kwenda kupigwa picha na kuchuliwa alama za vidole
ikushinde?” aliuliza Waziri huyo mwenye dhamana kubwa katika kusimamia
utekelezaji wa zoezi hilo.
Aidha amewataka viongozi wa Mikoa na wote wenye
dhamana katika kusimamia zoezi hili kuhakikisha wanashirikiana kwa karibu na
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa katika kuhakikisha wananchi wenye sifa
wanasajiliwa na kamwe pasiwepo wageni watakaojipenyeza kusajiliwa Vitambulisho
vya Taifa kama raia.
“Kwakuwa NIDA inatoa vitambulisho vya aina tatu,
cha Raia, Mgeni na Mkimbizi basi niwaombe wageni badala ya kufanya udanganyifu
wajisajili kwa hadhi yao kwani siyo dhamira ya Serikali kumfukuza yeyote lakini
kuwatambua Raia wake kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani” alisema
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme
amemhakikishia Mhe. Waziri mkoa wake uko tayari kusimamia na kuhakikisha
wananchi wote wenye sifa wanasajiliwa na kupata Vitambulisho ndani ya muda
uliopangwa na kwamba kamwe hata mvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo
katika utekelezaji wa zoezi hilo kwa wananchi; akiwakemea wanasiasa kuingiza
siasa kwenye zoezi la Usajili wananchi vitambulisho vya Taifa.
Mkoa wa Ruvuma wenye Wilaya 5 unakisiwa utawasajili
zaidi ya wananchi 900,000 katika zoezi lililopangwa kumalizika ndani ya miezi
mitatu. Tayari NIDA imekamilisha usambazaji wa vifaa na kutoa mafunzo kwa maafisa
ambao watatumika kuwasajili wananchi wa Ruvuma na viunga vyake.
Mikoa mingine inayoendelea na Usajili kwa sasa ni
Iringa, Mbeya, Njombe, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza,
Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Songwe, Lindi na Mtwara.
Comments
Post a Comment