- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
NAIBU Waziri wa Maji na
Umwagiliaji,Jumaa Aweso akisaini cha wageni kata ya Songea alipokuwa na
mkutano wa hadhara na wananchi wakati wa ziara yake.
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Jumaa Aweso akimwaga mchanga kwa ajili ya mradi huo
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua mradi huo wa maji
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Jumaa Aweso kulia akimuagiza Mkandarasi wa Maji mbele ya
Wananchi wa Tunduma kuhakikisha mradi wa maji unakamilika kwa wakati ili
wananchi waweze kupata huduma za maji .
NAIBU
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema hatasita kumchukulia hatua
mkandarasi yoyote ambaye atashindwa kukamilisha kwa wakati miradi ya maji
waliopewa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwasimamisha.
Lakini
pia ametoa wito pia wakandarasi wa magengeni kuacha kutumiwa kwenye maeneo
mbalimbali kwani wamekuwa ndio chanzo cha kupelekea miradi mingi kushindwa
kukamilika kwa wakati hali inayosababisha adha kubwa kwa wananchi.
Aliyasema
hayo baada ya kukagua mradi wa maji wa eneo Songea katika mji mdogo wa Tundyma
wilaya ya Momba mkoani Songwe ambao unatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya
Best One Company ambapo aliwataka kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa waledi
mkubwa ili uweze kuwa chachu ya mafanikio kwa wananchi hao.
Katika
mradi huo Serikali imetolea fedha bilioni moja kwa ajili ya mradi huo ambapo
Naibu Waziri huyo alizitaka zitumike kwa uangalifu mkubwa ili kuweza
kuukamilisha kwa lengo la kuondoa kero kwa wananchi .
Hata
hivyo alisema iwapo mradi huo utashindwa kukamilika kwa wakati hawasita
kumchukulia hatua ikiwamo kumsimamisha kazi kwani hawako tayari kuona uzembe
unafanyika wakati wananchi wana uhitaji mkubwa wa huduma hiyo.
“Labda
niwaambie kwamba sisi kama serikali nia yetu kubwa ni kuhakikisha wananchi
wanapata huduma ya maji safi kwenye maeneo yao lakini niwaambie kuwa pia
hatutamvumilia Mkandarasi yoyote ambaye akishindwa kukamilisha mradi huo kwa
wakati hasa huyo ambaye anatekeleza eneo hili “Alisema Naibu Waziri Aweso.
Naye
kwa upande wake,Mkuu wa wilaya ya Momba,Juma Irando ameitaka idara ya maji
wilayani humo kutowapa tenda wakandarasi wanaotuhumiwa kukwamisha juhudi za
serikali za kukabiliana na tatizo la maji kuhakikisha linakwisha
Hata
hivyo alisema inadaiwa kuwa baadhi ya miradi ya maji wilayani humo inashindwa
kukamilika kwa wakati kutokana na uwezo mdogo kitaalamu walionao baadhi ya
wakandarasi ambao wanakabidhi miradi (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Comments
Post a Comment