Featured Post

MHE MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA TAASISI YA UTAFITI (TPRI) MJINI ARUSHA KUWA WAZALENDO NA KUFANYA KAZI KWA WELEDI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza  maelezo ya namna ya ufanyaji kazi mara baada ya kutembelea Kitengo cha Unyunyuziaji wa Viuatilifu alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Kushoto) akitembelea baadhi ya maeneo ya Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa  akitumia mashine ya Kunyunyizia viuatilifu wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini maelezo ya namna maabara ya kupima masalia ya Viuatilifu inavyofanya kazi wakati alipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha, Leo 16 Disemba 2017.

Na Mathias Canal, Arusha

Watumishi wa serikali wanaofanya kazi katika Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika Ukanda wa Tropiki (Tropical Pesticides Research Institute-TPRI) wametakiwa kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa Weledi, Bidii na Nidhamu.

Kauli hiyo imetolewa Leo 16 Disemba 2017 na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Taasisi hiyo wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha.

Mhe Mwanjelwa aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii, Juhudi, Maarifa na Ubunifu kwani kufanya hivyo kutathibitisha matokeo chanya katika utendaji wao huku akiwapongeza kwa kufanya kazi kwa moyo na uvumilivu mkubwa pamoja na kuwepo kwa kadhia ya upungufu wa watumishi.

Sambamba na Taasisi hiyo kuwa na jukumu la kufanya utafiti, kutoa huduma za usajili na udhibiti wa viuatilifu, Mafunzo kuhusu visumbufu na kufanya hifadhi ya Bioanwai husika ili kuchangia uhakika wa chakula lakini pia ina jukumu la kuendelea na kudumisha mashamba darasa kwa ajili ya Utafiti na mafunzo kwa wadau hususani katika matumizi sahihi na salama ya Viuatilifu.

Aidha, Alimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TPRI) Dkt Margaret Mollel kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kusimamia Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na umakini wa Taasisi katika kufanya kazi zake katika kipindi cha miaka 10 ya utekelezaji wa muundo mkakati wa TPRI (2005-2015).

Alimsihi Mkurugenzi huyo anayesimamia Taasisi hiyo ya (TPRI) iliyotungiwa sheria na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (The TPRI Act No 18 of 1979) ikisimamiwa na Wizara ya Kilimo, kuongeza ufanisi zaidi katika usimamizi wa kazi kwa mujibu wa sheria na Taratibu za nchi.

Comments