- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
National
Arts Council
Tarehe:
27/12/2017
P.O. Box. 4779,
Ilala Sharif Shamba –Dar es Salaam.
Tel. 2863748/2860485
E-mail:
info@basata.go.tz
TAARIFA KWA UMMA
UKWELI KUHUSU KUTOFANYIKA KWA FAINALI ZA ‘MISS TANZANIA 2017’
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limekua likifuatilia kwa umakini mwenendo wa
shindano la Miss Tanzania na waandaji wake kampuni ya LINO Agency katika
kuhakikisha taratibu, kanuni na miongozo ya kuendesha matukio ya Sanaa nchini inazingatiwa.
Hivi
karibuni LINO wametoa taarifa ya kutokufanyika kwa shindano Miss Tanzania kwa
mwaka 2017 ambapo pamoja na sababu ya kukosa wadhamini wametaja kucheleweshewa
kibali na BASATA kama sababu ya kutokufanyika kwa shindano hili kwa msimu wa
mwaka 2017.
Tunapenda
kueleza kwamba sababu inayotolewa na LINO kwamba walicheleweshewa kibali na BASATA
si ya kweli na pengine imetengenezwa kuficha uhalisia wa changamoto za shindano
hili ambazo mara zote BASATA na hivi karibuni Waziri mwenye dhamana na sekta ya
Sanaa Mh. Dkt Harrison Mwakyembe amezieleza na kuzitolea maagizo.
BASATA
kama mtoa vibali vya matukio ya Sanaa nchini limeshangazwa na taarifa ya
kutokuwepio kwa shindano kwa msimu huu maana tayari lilikwishatoa kibali cha
muda kwa kampuni ya LINO ili kufanya maandalizi ya awali ya shindano hili
sambamba na kuandaa mshiriki wa shinda la Miss World 2017 lililomalizika hivi
karibuni mji wa Sanya nchini China amabapo Tanzania tuliwakilishwa na mshiriki
Julitha Kabete aliyekabidhiwa bendera chini ya uangalizi wa Wizara na BASATA.
Kibali
hicho cha muda ambacho kilitolewa mapema tarehe 08/09/2017 kinatoa fursa kwa
mwandaaji wa tukio la Sanaa kufanya maandalizi yote ya awali ya tukio la
Sanaa/Burudani huku akiwa chini ya uangalizi maalum wa kukamilisha taratibu
mbalimbali za msingi kwa ajili ya kupewa kibali cha mwisho cha tukio husika hivyo
kampuni ya LINO haina sababu yoyote ya kutaja kibali cha BASATA kama kikwazo
cha kufanyika kwa shindano la Miss Tanzania mwaka huu maana tayari walikua na
kibali hiki cha muda kinachowapa fursa za maandalizi yote ya awali ya shindano
Tunazidi
kutoa wito kwa waandaaji wote wa mashindano/matukio ya Sanaa kuzidisha weledi
na zaidi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kuendesha matukio ya Sanaa
kama zinavyo fafanuliwa katika vikao vya mashauri mara kwa mara. Aidha tunazidi
kusisitiza umuhimu wa kujenga taswira chanya kwa matukio ya Sanaa na kuyajengea
uendelevu ili kuvutia wawekezaji zaidi na kuyapa mvuto mkubwa wa kibiashara.
BASATA
kama msajili na mtoa leseni katika matukio ya Sanaa tutaendelea kuzingatia
weledi na kutoa huduma zetu kwa haraka, ubora na kuzingatia kwa umakini mkubwa
sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji matukio ya Sanaa ambazo kwa pamoja
wadau wote tumeziridhia.
KATIBU MTENDAJI
BARAZA
LA SANAA LA TAIFA - BASATA
Comments
Post a Comment