Featured Post

DC, MBUNGE MUHEZA WASHIRIKIANA NA WANANCHI KUANZA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA HIYO

 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani humo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Like Gugu wakishuhudia tukio hilo.
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akichimba mtaro kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo eneo la Lusanga wilayani humo kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo,Like Gugu
 Sehemu ya wananchi wakishiriki katika uchumbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Muheza Mkoani Tanga
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akishiriki kubeba tofali kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali itakayojengwa eneo la Kijiji cha Lusanga wilayani Muheza
 Sehemu ya wadau wa maendeleo wilayani Muheza wakishiriki kwenye zoezi la ubebaji wa matofali wilayani humo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu wa pili kutoka kulia wakipokea mifuko 600 ya saruji kutoka kwa kampuni ya Lucky Cement ya Kisarawe Mkoani Pwani kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto  ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
 Sehemu ya shehena ya saruji ambayo ilishushwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kupokea saruji hiyo ambapo aliishurku kampuni hiyo huku akiyataka makampuni mengine yaliyopo mkoani hapa kuunga mkono jitihada hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu
 Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu akizungumza katika halfa hiyo ambapo aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia ujenzi huo huku akiyataka makampuni mengine kuiga mfano huo
Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya akizungumza na waandishi wa habari kuhusu azma yao ya kusaidia mifuko ya saruji 600 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Muheza kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza,Balozi Adadi Rajabu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muheza,Like Gugu 
 
MKUU wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo,Mbunge wa Jimbo hilo,Balozi Adadi Rajab na wakazi wa wilaya hiyo  wakishirikiana kwa pamoja wameanza kuchimba msingi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya katika Kijiji cha Lusanga Kata ya Lusanga ambayo itasaidia kuondoa changamoto ya kutokuwepo kwa kipindi cha miaka 37.

Hatua ya viongozi hao ina lengo la kuandika historia tokea wilaya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1974 ambapo wananchi walikuwa wakitegemea kupata huduma za matibabu kwenye hospitali ya Teule Muheza kutoka maeneo mbalimbali kabla ya kufikiria kuanzishwa kwa hospitali hiyo ambayo itakayogharimu zaidi ya bilioni 11.

Akizungumza wakati akishiriki zoezi la uchimbaji wa mtaro wa Hospitali hiyo na kupokea mifuko ya saruji 600 ya Lucky kutoka kwa Kampuni ya kuzalisha Saruji ya Kisarawe, Mhandisi Mwanasha alisema waliamua kufanya hivyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya huduma ya afya ambayo ilimlazimu wakati ameteuliwa kuiongozi wilaya hiyo kukutana na wadau kuweza kuona namna ya kuweka mikakati ya kupatikana kwake.

Aidha kutokana na kuwepo kwa hospitali ya wilaya walikuwa wakilazimika kutimia hospitali ya teule Muheza tokea ilipoanzishwa lakini imeonekana kuzidiwa na watu wanaohitaji huduma hasa ukizingatia pia zahanati na vituo vya afya vipo vichache huku wananchi wakiongezeka.

“Nilibaini changamoto ya hospitali ya wilaya wakati nilipokuwa nikifanya vikao kwa kuzunguka kata zote nikaona tatizo la huduma ya afya ni kubwa sana na hivyo kuonekana kuna haja ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Muheza lakini hata kwenye baraza la madiwani suala hilo lilizungumzwa”Alisema

Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya kufikiria wazo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo waliona wafanya mazungumzo na Agro Tan ambao wanamiliki Shamba la Muheza Estate ambao walikubali kutoa eneo lao la ekari 100 kwa ajili ya ujenzi huo.

Awali akizungumza katika eneo hilo,Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema juzi ilikuwa  ni siku muhimu sana kwao kutokana na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye msaragambo kwa nia ya kujengwa hospitali ya wilaya ambacho kilikuwa kilio chao kwa muda mrefu.

 Alisema waliamua kuanzisha mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo baada ya kuona huduma ambazo zilikuwa zikitolewa katika hospitali ya Teule Muheza kuelemewa kutokana na watu kuongezeka huku maradhi yakiwa mengi kila wakati na ndio walipoamua kuchukua uamuzi huo.

Mbunge huyo alisema wananchi wa wilaya hiyo waliposikia mipango ya kuwepo kwa ujenzi huo walianza kujitolea fedha kiasi cha elfu mbili ikiwemo kushiriki kwenye uchimbaji wa msingi wa ujenzi wa hospitali hiyo tokea alfajiri wakiunga mkono juhudi za serikali.

“Lakini pia nisema tunawashukuru kampuni ya Lucky Cement kwa kutukabidhi mifuko 600 ya saruji na tunategemea pia kuvitumia viwanda vilivyopo mkoani Tanga kwa lengo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa hospitali ya wilaya yetu tunavifaa vya kutosha vya kuanzia tutaanza na baadae wataingiza kwenye bajeti kuiomba serikali iwasaidie”Alisema Mbunge huyo

Kwa upande wake,Meneja Masoko wa Kampuni ya Lucky Cement iliyopo Kisarawe,Emanuel Muya  alisema wao kama wadau wa maendeleo waliguswa na kuamua kuchangia ujenzi wa hospitali hiyo ili kuwasaidia wananchi kuondokana na changamoto za huduma ya afya katika wilaya hiyo.

Alisema kwa kutambua thamani ya maendeleo katika nchi ndio sababu kubwa iliyowasukuma kuamua kusaidia saruji hiyo kwa ajili ya kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali hiyo ambapo itakapokamilika itawasaidia kuwaondolea changamoto wananchi.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Comments