Featured Post

WATUMISHI WA AFYA BADO WANAHITAJIKA NCHINI

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya majaribio ya kuchunguza wadudu kwa kutumia hadumini iliyopo kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba dkt. Aloyce Musika amesema kuwa wahitimu wanatakiwa kujiendeleza na elimu ili kuongeza kiwango cha elimu na kuwa wabobezi katika kutoa huduma za afya zilizo bora na kwa uhakika nchini.

“Wahitimu waliotunukiwa vyeti leo hii wasiwaze kuajiriwa tu bali wafikirie kuwa msaada wa kutoa huduma za afya katika jamii huku wakifikiria kuongeza ujuzi zaidi katika taasisi mbalimbali hapa nchini ili watoe huduma za afya kwa uhakika” alisema Dkt. Musika

Mbali na hayo msoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Saleh Said ambaye ni Muhitimu wa fani ya Udaktari ngazi stashahada amesema kuwa anaiomba Serikali kuangalia kwa ukaribu na kuweka utaratibu pindi wanafunzi wanapomaliza mafunzo yao kwenye masula ya afya waweze kupata ajira kwa haraka.
Naibu Waziri wa afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya Chuo Cha Afya na Tiba KAM kwa kuwatunukia wahitimu 600 Shahada na stashahada ya fani mbalimbali katika kada mbalimbali za sekta ya afya.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wa kwanza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wataalam wa chuo cha Afya na Tiba KAM kuhusu vifaa vinavyotumika maabara kwenye moja ya maabara ya chuo cha Afya na tiba cha KAM wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM hawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM dkt. Aloyce Musika akiongea na wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM whawapo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

Comments