- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aakiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz na Ramon Abecia walipoianza safari ya kuelekea kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto) na Ramon Abecia (Kulia) walipofika katika kituo cha kupumziki cha Horombo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal akiendesha baiskeli katika eneo la Saddle wakati wa kuekelea kituo cha Kibo .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal akikokota baiskeli yake katika eneo lenye mawe wakati akiekelea kituo cha Kibo
Muongoza Watalii,Ally Chuwa akitoa msaada wa kufunga viatu kwa Ramon Abecia wakati akielekea kituo cha Kibo.
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal akiwa katika kilele cha Uhuru mara baada ya kufanikiwa kufika huku akiendesha baiskeli .
Mpanda milima mashuhuri Duniani kwa kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal (katikati) akiwa na wenzake wawili ,Eduardo Pascuaz(kushoto) na Ramon Abecia (Kulia) katika kilele cha Uhuru walipoanda kwa kutumia baiskeli .
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadi za Taifa ,(TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza mara baada ya wageni hao kushuka baada ya kufanikiwa kufika kilele cha uHuru kwa kutumia Baiskeli.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
limesema litafikiria matumizi ya Boda boda na Bajaji kwa wageni watakao hitaji
kutembelea Hifadhi zake endapo yatajitokeza maombi ya kutosha kuhusu matumizi
ya vyombo hivyo.
Hatua hiyo inatokana na bidhaa mpya ya
Utalii wa kutumia Baiskeli iliyoanzishwa hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa
za Mlima Kilimanjaro na Arusha kuanza kuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi
mbalimbali walioanza kufanya utalii wa Baiskeli.
Miongoni mwa watali hao ni pamoja na
mpanda milima mashuhuri Duniani kwa
kutumia Baiskeli ,Juanito Oiarzabal aliyeweka rekodi ya
kuwa Mhispania wa kwanza kupanda Mlima Kilimanjaro huku akitumia saa 31 akiendesha
baiskeli katika siku tano hadi kufika kilele cha Uhuru.
Juanito na wenzake wawili , Eduardo Pascuaz na Ramon
Abecia waliianza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli ,wakianza
safari yao kupitia lango la Kilema ,aina hi ya utalii ikiwa ni bidhaa mpya
katika Milima huo mrefu kuliko yote barani Afrika.
Aina hii mpya ya utalii
ambayo kwa sasa imeanza kushika kasi katika Hifadhi za Taifa ,za Mlima
Kilimanjaro,Arusha na Saadan inatokana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
kuendelea kupanua wigo wa vivutio katika Hifadhi zake 16,
Meneja Mawasiliano na
Mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete amesema hatua ya Juanito na wenzake kufika katika kilele cha Uhuru inaashiria kuanza
kufunguka kwa aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi za Taifa .
Shelutete amesema namna
ambavyo Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) limekuwa mstari wa mbele katika
kubuni aina mpya ya bidhaa za utalii ili
kushindana na nchi nyingine duniani katika uuzaji wa safari kwa watalii.
Kwa upande wake Juanito
Oiarzabal ambaye amepata ulemavu wa kukatika vidole kutokana na barafu katika
Milima mbalimbali aliyopanda amesema changamoto aliyokutana nayowakati wa
kupanda mlima ni kuzoea hali ya hewa yam lima ambayo imekuwa ikibadilika kila
mara.
Mkurugenzi wa kampuni ya
Safari Bike Africa iliyoratibu changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa
kutumia Baiskeli kwa wageni hao,Mario Martos amesema kampuni yake imekusudia
kuleta mabadiliko katika sekta ya utalii kwa kufanikisha safari za watalii wa
kutumia baiskeli.
Shirika la Hifdhi za Taifa
(TANAPA) limejipanga kuhakikisha usalama wa hali ya juu kwa wageni watakaofanya
aina hii mpya ya utalii katika Hifadhi zake kwa kuwa na taahadhari sambamba na
waongoza wageni waliobobea katika kazi ya Utalii.
Mwisho.
Comments
Post a Comment