- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mhubiri anayetumia nyoka nchini Afrika
Kusini, Penuel Mnguni, amewalisha mende ndugu wawili
MUHUBIRI mashuhuri anayetumia nyoka nchini Afrika Kusini
Penuel Mnguni amewalisha mende ndugu wawili katika mkusanyiko wa kanisa lake
akidai kwamba wadudu hao walibadilika na kuwa jibini kwa mmoja wao na kiungo
kwa mwengine.
Kisa hicho kinajiri takriban miezi mitano baada ya Mnguni
katika ibada iliyoandaliwa na Muhubiri wa Nigeria TB Joshua, na kukiri
kulingana na Bwana Joshua kwamba kuwalisha watu haijaandikwa katika Biblia.
Kanisa la bwana Mnguni lilichapisha katika mtandao wa
facebook kuhusu kisa hicho cha kula mende mapema mwezi huu akisema kuwa
muhubiri huyo alimwita mende kuja katika kanisa hilo.
Baadaye aliwaita wafuasi wa kanisa hilo kujitokeza mbele na
kula....ndiposa ndugu wawili walijitokeza na kula pamoja...na walipokuwa wakila
bwana Charles alihisi anakula jibini huku Bwana Eric akihisi kula kiungo,
chapisho hilo lilisema.
Huku akizungumza maneno haya ''uwezo wa mungu uliwagusa wote
wawili, kwa kuwa walipo'' , aliongezea.
Kanisa hilo pia liliripoti katika chapisho jingine kwamba
muhubiri huyo aliliombea uwa la sumu , na baadaye mfuasi mmoja alilila ua hilo
pekee na kulimaliza.
Nabii huyo aliyejitangaza alizua utata nchini Afrika Kusini
2015 baada ya kushutumiwa kwa kuwalisha nyoka wafuasi wake.
Mashtaka dhidi ya Mnguni yaliowasilishwa na shirika la
kuzuia ukatili dhidi ya wanyama ,yalitupiliwa mbali mnamo mwezi Julai 2015
kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Comments
Post a Comment