- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaofanya
shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya
Sirari , wakati wa ziara ya kikazi aliombatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Dkt. Anna Makakala (watatu kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo.Lengo la ziara hiyo ni kukagua shughuli
mbalimbali zilizopo chini ya idara za wizara na kukagua mipaka iliyopo katika mkoa huo.Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala, akizungumza na wananchi wanaofanya
shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya kikazi
ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya mkoa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akijibu baadhi ya hoja zilizoulizwa na wananchi wanaofanya
shughuli zao katika Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari, wakati wa ziara ya
kikazi ya Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
(wapili kulia), akiambata na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala
(kulia) Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala (wapili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorius Luoga (kulia), wakisikiliza maswali ya
mmoja wa wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka wa Tanzania na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye
lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Naibu
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji,Dkt. Anna Makakala( kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima(watatu
kulia) wakisikiliza maswali ya mmoja wa
wananchi wanaofanya shughuli karibu na kituo cha Mpaka Tanzanua na Kenya Sirari , wakati wa ziara ya kikazi yenye
lengo la kukagua mipaka iliyopo ndani ya mkoa huo. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Na Abubakari Akida-WMNN
NAIBU
Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
amewataka wananchi na wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao karibu na Kituo
cha Mpaka wa Sirari unaotenganisha nchi za Tanzania na Kenya kuhakikisha
wanashirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Mara kudhibiti matukio ya uhalifu kwa
kutoa taarifa za wahalifu hao kwa jeshi hilo.
Hayo
ameyasema akiongea na wananchi wakati wa ziara ya kikazi katika mkoa wa Mara,
ikiwa na lengo la kutembelea mipaka iliyopo katika mkoa huo inayotenganisha
nchi ya Tanzania na nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo katika ziara hiyo
aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, Kaimu
Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibiche na Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
“Tumekuwa
tukipata taarifa wananchi wa hapa kushirikiana na wahalifu katika kupitisha
mali za magendo hapa hasa wakitumia vijana wanaoendesha bodaboda kupitisha
mizigo yao na kuripotiwa matukio mbalimbali yanayohatarisha usalama wa raia
wetu, natoa wito kwa wananchi wa hapa kushirkiana na jeshi la polisi kudhibiti
matendo hayo ya kihalifu,” alisema Masauni
Aidha,Naibu
Waziri Masauni amewataka wananchi hao kuacha mara moja tabia inayokua kwa kasi
katika eneo hilo ya kulizuia Jeshi la Polisi kufanya shughuli zake na endapo
atabainika mtu yoyote atakumbana na mkono wa sheria huku akitoa ushauri kwa
jeshi kuzifanyia utafiti taarifa zitakazoletwa ili kuepuka kumuonea mtu.
Akizungumza
na wananchi hao Kamishna Jenerali wa
Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, amewataka wananchi hao kupeleka taarifa za
wahamiaji haramu pindi watakapowagundua ili kuweza kudhibiti tatizo la
wahamiaji hao kuingia nchini huku akiweka wazi viwango vya udhibiti vilivyoweka
na idara yake kuzuia wahamiaji haramu kuingia nchini.
“Idara
ya Uhamiaji kupitia wawakilishi wetu mkoani hapa tupo tayari na tunaomba mtu
yoyote mwenye taarifa za wahamiaji
haramu azifikishe kwenye ofisi ya uhamiaji nasi tutazifanyia kazi kwani
tushapunguza tatizo hilo na tuko katika jitihada za kulimaliza kabisa,” alisema
Dk. Makakala
Akizungumza
kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taida (NIDA),
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Alphonce Malibiche,
alisema NIDA imezindua zoezi la usajili wa vitambulisho kwa wakazi wa Mkoa wa
Mara na wanatarajia kumaliza zoezi hilo mapema ili wananchi wa Mkoa huo na
wilaya zake wawe na vitambulisho vya Taifa vitakavyozuia baadhi ya changamoto
lakini lengo kubwa ni kuhakikisha kila Mtanzania anakua na Kitambulisho cha
Taifa.
Comments
Post a Comment