- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
UGONJWA wa
Sotoka ya Mbuzi au 'Tauni ya Mbuzi na Kondoo' (Peste des Petits
Ruminants – PPR) husababishwa na virusi na hushambulia kondoo na mbuzi
ukiwa na dalili zote kama Sotoka (rinderpest) inayoshambulia wanyama
kama ng'ombe, nyati, ngamia na wengineo.
Kwa
taarifa tu ni kwamba ugonjwa wa Sotoka (rinderpest) ulitokomezwa duniani
mwaka 2011 na Shirika la Afya Duniani (WHO) kufanikiwa kuudhibitisha.
Ugonjwa wa
PPR ulisambaa sana miaka ya 1980 na kuathiri sehemu kubwa ya
Afrika na duniani kote ambapo huwashambulia zaidi mbuzi kuliko kondoo.
Kwenye
ng'ombe unaweza kuukuta kwa kupima damu, lakini kwa kawaida ng'ombe
hawataonyesha dalili wala kuusambaza ugonjwa wa PPR.
Ugonjwa
huu unaweza kuua wanyama kwa kiwango cha mpaka asilimia 100% kutegemeana
na umri wa wanyama, afya, lishe na kuchoka kutokana na kufuata malisho umbali
mrefu sana.
Kwa
wanyama wenye umri kati ya miezi 4 - 8 hali huwa mbaya zaidi na pia
wanyama wenye maradhi mengine ni rahisi kushambuliwa kutokana na kinga kuwa
chini.
KUSAMBAA
Ugonjwa PPR
husambaa kwa njia ya kugusana na virusi vya ugonjwa huu huwa kwenye
matongotongo, makamasi, mate na kinyesi cha wanyama.
Kwa hiyo
mnyama mwingine akigusa kimoja kati ya hivi ataambukizwa ugonjwa huu.
DALILI
Dalili kwa
wanyama ni kama kuharisha.
-Homa kali
kati ya siku 5 – 8
-Mnyama
hutoa makamasi ya kawaida na baadaye kubadilika rangi na kuwa ya kahawia
-Kuziba
pua na kusababisha ugumu wakati wa kupumua
-Michubuko
kwenye pua na midomo
-Wanyama
kutoona vizuri kutokana na matongo tongo kwenye macho
-Mnyama
kuishiwa maji mwilini na pia mimba kutoka.
Matongotongo
UCHUNGUZI
Uchunguzi
wa kitaalam ufanywe na maofisa ugani wa mifugo ili kugundua uwepo wa ugonjwa huo
kwa kuukagua mwili kuona uwepo wa makamasi ya kahawia.
Watakagua pia
kuona kama mnyama anatoa kinyesi cha maji maji chenye harufu mbaya.
Pia
watachunguza njia ya hewa, chakula na sehemu ya juu ya mdomo (hard palate). Kwenye
utumbo wa mnyama aliyekufa kwa ugonjwa huo huwa na mistari kama ya pundamilia.
Kuvimba
kwa mitoki na usaha kwenye mapafu ni mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kugunduliwa.
Baada ya
hapo damu ya mnyama itachukuliwa na kupelekwa kwenye maabara ikisafirishwa
kwenye hali ya ubaridi (refrigeration).
Utumbo wa mbuzi aliyekufa kwa Sotoka.
DAWA
Ugonjwa wa
PPR hauna dawa ila kwa wanyama watakaoweza kuhimili dawa za kuua bakteria (antibiotics) zitasaidia kuzuia
mashambulizi ya juu dhidi ya bacteria hao.
KINGA
Chanjo ya
ugonjwa huu ipo. Unachotakiwa kufanya ni kuwasiliana na maofisa ugani wa mifugo
katika eneo lako.
Chanjo ni
muhimu mara moja kwa mwaka kabla ya kuanza kwa mvua za masika.
Tenga
wanyama wapya wiki tatu kabla ya kuwachanganya na wengine.
Tenga
wanyama wagonjwa na wazima mara ugonjwa unapoibuka.
Osha
mabanda yako kwa dawa za kuulia virusi kama virukill au tumia dawa za madoa kama JIK kiasi cha lita moja
kwa lita 30 za maji kisha pulizia.
Comments
Post a Comment