Featured Post

RITTA KABATI AKERWA NA MIMBA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA KWAKILOSA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea na wanafunzi, wazazi na walimu wakati wa mahafali ya kidato cha nne mwaka huu 2017 katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo katika Manispaa ya Iringa.
Baadhi ya wanafunzi na wazazi walihudhuria sherehe za kuhitimu kwa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi cheti mmoja ya wanafunzi wa kike aliyehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Kwakilosa

Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekerwa na uwepo wa mimba za utotoni katika shule ya sekondari ya Kwakilosa iliyopo kata ya Mwangata manispaa ya Iringa kwa kuwa kitendo hicho kinachosababisha kushuka kwa elimu katika shule hii.

Akizungumza wakati wa shererhe za kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka huu Kabati alisema kuwa amesikitishwa kusikia kila mwaka kuna wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito.
“Jamani tumekuwa tukitoa elimu kila mara juu ya madhara yanayotoka na upatikanaji wa mimba za utoto za hiii shule imekuaje kila mwaka wanafunzi wanapata mimba hii haikubariki katika jamii kabisa maana hawa wanafunzi ndio tegemeo la taifa kwa sasa” alisema Kabati

Kabati aliwataka wazazi na walimu kuwalinda wanafunzi wa kike ili wasikumbane na ardha ya kupata mimba wakiwa watoto wadogo kwani kunapoteza muelekeo wa maisha yao na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

“Haiwezekani kila mara wazazi mnakuwa wa kwanza kuwa chanzo cha kuwaharibu watoto na kwanini wazazi mnafanya hivyo maana watoto hawa ndio watakao wasaidia hapo baadae ndio maana mkiwa mmezeeka kwa hiyo ndio watakuwa msaada katika maisha yenu naombeni muwatunze watoto wenu” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwataka wanafunzi wote mkoani Iringa na Tanzania kwa ujumla kuacha kufanya mapenzi wakiwa na umri kama wao hivyo wanapaswa kujilinda ili kufikia malengo yao waliojiwekea na walidhike na kipato walicho nacho wazazi wao.

“Hivi kaka mimi ningeanza mapenzi nikiwa na umri kama wenu unafikiri ningefikia malengo haya niliyonayo hivyo nawaomba msifanye mapenzi mkiwa na umri mdogo ili baadae mje kufikia malengo yenu” alisema Kabati

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Hudson Luhwago aliwatupia lawama wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo kwa kutowalea katika malezi mazuri wanafunzi hao.

“Yaani kabisa mzazi anakuja na wanafunzi anamuombea ruhusa kuwa walikuwa fiesta wote hivyo mtoto amechoka hawezi kuja shule hii ni aibu na ukweli unaoendelea kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule hii” alisema Luhwago

 Luhwago alisema kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wanawanaume zaidi ya watano na wazazi wanayajua hayo lakini wanashindwa kuwakemea watoto wao na ndio maana wanakuja shule wakiwa na kiburi hata kwa walimu.

“Wanafunzi hawa wanaomaliza hitimu shule leo walikuwa wanakiburi kwa sisi walimu hadi ikabidi tukae kama wanalimu tuwajadili lakini chanzo chote ni malenzi mabaya wanayoyapata kutoka kwa baadhi ya wazazi au walezi wao” alisema Luhwago

Akisoma risala kwa mgeni rasmi makamu mkuu wa shule Praygod Makongwa alisema kuwa hadi sasa kuna mwanafunzi ameachishwa shule akiwa kidato cha kwanza kwa sasbabu ya kuwa mujamzito na hata hawa wanaohitimu hii leo mwenzao mmoja alikatisha masomo akiwa kidato cha pili kwa kuwa na ujauzito.

“Sisi kama walimu wa shule hii tushazoe kuona wanafunzi wanakatisha masomo kwa ajili ya kupata mimba na ukiangalia kwa umakini walimu tunawalea wanafunzi kwa maadili yanayotakiwa tatizo lipo kwa wazazi hao unakuta mtoto na mzazi wapo disco pamoja wanakunywa pombe pamoja sasa hapo utapata matokeo gani?” alisema Makongwa


Lakini Makongwa alisema kuwa shule imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inajenga majengo ya mabweni kwa wanafunzi ili kumaliza tatizo la mimba za utoto na kuboresha elimu ya shule ya sekondari ya Kwakilosa.

Comments