- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Ng'ombe aliyekufa kutokana na Ndigana Kali
UGONJWA wa Ndigana Kali au
kitaalam East Coast Fever (ECF)
hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, nyati na nyati wa India wakaao
kwenye maji (Water Buffalo).
Ugonjwa huu husababishwa na
vimelea (protozoa) vijulikanavyo kama
Theileria parva ambavyo husambazwa na
kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanao kama Rhepicephalus Appendiculatus.
Kwa kawaida, ugonjwa huu
usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali
kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine.
Ndigana Kali ni ugonjwa
ulioenea sana hapa nchini kwetu na Afrika Mashariki, ambapo ng’ombe huanza
kuugua siku 10 – 25 (wastani siku 14) tangu kuambukizwa.
DALILI ZAKE
-Joto kali hadi kufikia 42c
badala ya joto la kawaida la ng’ombe la nyuzijoto 38c
-Homa kali
-Mnyama kushindwa kupumua
vizuri
-Kukohoa
-Kuharisha
-Kuvimba matezi ya shingoni
-Manyoya ya mgongoni
husimama muda wote na huwa na rangi ya udongo (brown) kwa mbali
-Kutoa makamasi laini
-Kupe aina ya rephicephalus appendiculatus wataonekana
ndani ya masikio ya mnyama (sio lazima)
-Mnyama hushindwa kula
vizuri
-Pua (muzzle) huwa kavu
bila unyevu unyevu.
MATIBABU
Mnyama inabidi apigwe
sindano ya dawa za PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20
(soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada ya siku moja
kupita, yaani akichomwa leo unarudia dozi kesho kutwa.
Pia mnyama achomwe dawa ya OTC
20% kipindi chote cha matibabu.
Dawa aina ya BUTALEX ni
maarufu sana hapa nchini kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huu, ni muhimu
dalili za mwanzo zinapoonekana kumtaarifu mtaalam wa mifugo na ikithibitika ni
Ndigana Kali tiba ianze mara moja ikiambatana na OTC 20% ili kushusha homa.
KINGA
Kinga kubwa ni kuogesha
mifugo yako mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua
wadudu wa mifugo.
Dawa ijulikanayo kama PARANEX
hupatikana katika maduka yote ya kilimo na mifugo. Dawa nyingine nazo zinafaa
kuogeshea kwa kufuata masharti ya mtengenezaji.
Comments
Post a Comment