- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Ng'ombe anayeumwa Nagana.
NAGANA au
kitalaam Trypanosomiasis ni ugonjwa
ambao hushambulia karibu mifugo yote na pia binadamu. Kwa
binadamu ugonjwa huu hujulikana kama malale.
Ugonjwa
huu husababishwa na vimelea vya protozoa vijulikanavyo kama Trypanosoma evansi na husambazwa na
mbung'o au ndorobo (glossina spp).
Mbung'o akimuuma mtu.
Vijidudu
hivi vikimuingia mnyama vinafyonza kiasi kingi cha sukari kwenye mwili wa
mnyama na kuharibu chembe nyekundu za damu na kusababisha upungufu
mkubwa wa damu kwa mnyama husika.
DALILI
DALILI
-Ugonjwa huu kwa ng'ombe
unaweza usiwe hatari, wa kawaida au hata kuwa sugu na kuleta madhara
makubwa ikiwemo kifo.
-Joto la
mnyama hupanda hadi kufikia nyuzijoto 39C – 41C
-Mnyama
hupata tabu kuona huku akitoa machozi mengi kama anayelia
-Uzalishaji
wa maziwa hupungua ghafla kwa kiasi kikubwa
-Mnyama
hupumua kwa tabu kwa kutumia nguvu
-Mnyama
huonyesha kuchanganyikiwa akili, anaweza kutembea kwa mduara, kupiga pika
kichwa kwenye mabanda au chochote na mnyama huweza kupoteza fahamu
-Baadhi ya
wanyama wajawazito huweza kutoa mimba, hii ni kwenye ile hali ya ugonjwa sugu
ambao hushambulia pole pole
-Kuvimba
kwa matezi
-Manyoya
ya ng'ombe mgongoni wakati wa asubuhi yana kuwa yanang'aa fulani jua likiwaka,
ila inahitaji uonyeshwe na wataalam kwanza.
UCHUNGUZI
Maafisa
ugani wa mifugo watachukua sampuli za damu kutoka kwenye mkia au sikio la
mnyama na vijidudu kuonekana kwa darubini ya umeme mkali kabla ya damu kukauka,
pia njia ya kimaabara ya GIEMSA itasaidia kwa uchunguzi zaidi wa
kimaabara wadudu wanaweza kupandikizwa kwenye sungura, panya na simbilisi/pimbi
na baadae njia ya PCR, ELISA kutumika kuangalia vichochezi vya mwili.
TIBA
Kwa mifugo
kama ng'ombe, mbuzi, kondoo, jamii ya farasi, mbwa na paka dawa kama diminaphen, diminakel hutumika kutibu
ugonjwa huu, kwa upande wa binadamu sifahamu dawa gani inatumika.
KINGA
- Kuna
njia ya kitaalam ijulikanayo kama sterile male technique, ambapo madume ya
mbung'o hupigwa na mionzi ya gama na kushindwa kuzalisha yanapo panda, hii
husaidia sana kwa sababu majike ya mbung'o hupandwa mara moja tu katika maisha
yao wakati madume haya tasa huendelea kupanda majike tofauti tofauti.
- Dawa zinazomika kutibu
ugonjwa huu zinaweza kukinga wanyama kama watapigwa kila baada ya miezi mitatu
na mara 4 kwa mwaka.
- Ng'ombe
wanaojulikana kama N'DAMA wanaopatikana Afrika Magharibi wanastahimili sana ugonjwa huu.
Comments
Post a Comment