Featured Post

MIAKA 100 YA SKAUTI: MKUU WA WILAYA SOPHIA MJEMA ATOA AGIZO LA UANZISHWAJI WA KLABU ZA SKAUTI KILA SHULE MANISPAA YA ILALA


Mkuu wa wilaya akizindua mapango wa mawasiliano kwa njia ya redio maalumu njia ya upepo na inteneti  kwa skauti  ‘Jamboree on the Air (JOTA).

Mkuu wa wilaya ya ilala Sophia Mjema Akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake akiwa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wilaya ya ilala.


Na Michael Utouh


Mkuu wa wilaya ya Ilala ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya akikagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili yake na wanafunzi wanaopata mafunzo maalumu ya scout alipofika kwa ajili ya kufunga makambi yao ya mafunzo siku ya leo.


Mkuu wa wilaya akiwahutubia wanafunzi wa scout.

Mmoja wa wakilishi wanafunzi wanaopata mafunzo ya scout wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi.
Mkuu wa wilaya akikapewa maelekezo juu ya mpango anzilishi wenye lengo la kumkomboa mwana scout na baadhi ya mambo mengi kama vile Elimu nk.
Akitembezwa pamoja na kukagua baadhi ya makambi ambayo wameyaweka wanafunzi hao kwa ajili ya mafunzo yao.



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema  amemuagiza afisa elimu wa wilaya ya Ilala kuhakikisha kila shule inafanya uandikishaji wa wanafunzi kwa ajili ya mafunzo ya vikundi vya skauti nakila shule ihakikishe inatoa mwalimu mmoja kwa ajili ya kusimamia vikundi hivyo.

Mjema ameyasema hayo katika kuadhimisha miaka 100 ya skauti tangu kuanzishwa kwake 1917 sambambana kuzindua wiki mawasiliano ya anga kwa njia ya upepo na inteneti  kwa skauti  ‘Jamboree on the Air (JOTA), Jamboree on the Internet (JOTI)’yaliyofanyika katika shule ya Sekondari Pugu Jijini Dar es Salaam.


“Ikama ya walimu wa skauti ni ndogo natoa agzio kwa afisa elimu kufanya uandikishaji wa skauti wakike na wakiume katika kila shule na kuhakikisha kila shule kunakuwa na mwalimu mmoja ambaye atakuwa anawafundisha skauti hao” Amesema Mkuu wa wilaya



DC Mjema ameeleza kuwa skauti wengi ni vijana wakifundishwa maadili mema Tanzania itakuwa ni yenye umma bora na watu wake watakuwa na uzalendo na Taifa la Tanzania.

“Skauti wengi ni Vijana hivyo ni wajibu wao kutengeneza ulimwengu bila madawa ya kulevya, bila maovu , kutengeneza skauti wazalendo wenye tija na Taifa la Tanzania, pia wanapopata fursa mbalimbali za nje ya nchi wasisite kuitangaza Tanzania kwa kueleza mema ya Tanzania ikiwemo Amani, Muungano na Rasilimali zilizopo” Amesema.

Pia DC Mjema ametoa wito kwa watoto na skauti wote pindi wanapoona matukio ya kidhalilishaji au kufanyiwa watoe taarifa kwa mamlaka kwa mamlaka husika kwani serikali ipo kwa ajili yao na itawalinda.

“Wenyeviti wa Serikali za Mtaa, Wakuu wa Wilaya, Mawaziri, mpaka ngazi ya juu ya Rais chini ya Rais John Pombe Magufuli tutahakikisha tunazilinda na kuzitetea haki za mtoto hivyo wasiogope kutoa taarifa za unyanyasaji kijinsia hata kama wakitishiwa maisha yao” Amesema.

Katika hatua nyingine DC Mjema amehaidi kushughulikia moja ya changamoto iliyotolewa na wawakilishi wa uongozi wa skauti kuhusiana na eneo la kambi na eneo kwa ajili ya kilimo ambapo amewahakikishia uwepo wa maeneo hayo kwa kumuagiza Mkurugenzi kuwapa kipaumbele pale watakapo ainisha maeneo kwa ajili ya viwanda vidogo kwani kufanya hivyo ni kuwakwamua kiuchumi.

“Namuagiza Mkurugenzi kushughulikia suala la eneo la kilimo, pia ni vyema mkaja ofisini kwangu siku ya Alhamisi ili niwakutanishe na Afisa Maendeleo kwa ajili ya kujadili na kufikia malengo yenye tija kwa skauti na taifa kwa ujumla” Amesema.



Comments