- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi
amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na kama unavyo muona akiwa anashusha safuji hiyo kutoka kwenye gari.
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi
amekabidhi mifuko ya saruji akiteta jambo na wananchi waliofika katika eneo hilo alipokuwa akikabidhi saruji hizo.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi amekabidhi mifuko ya saruji 130 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule ya msingi ya Maarifa,kinyanmbo na zahanati ya Rungemba kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la
kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kuel kuhakikisha natimiza azma
yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini.
“Nimetoa
mifuko 130 ya saruji kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi wa madarasa katika shule
mpya ya Maarifa na zahati ya Rungemba hii ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji
nyingine ili kulifanya jimbo la Mafinga Mjini kupata maendeleo kwa kasi”
alisema Chumi
Chumi
alisema kuwa halmashauri ya Mji wa Mafinga imeshaanda mpango kabambe ambao
utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku mji ukiwa
umeshapangiliwa jinsi gani ya kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hii.
“Ukiangalia
miji mingi inakuwa bila kuwa na mpango kabambe kitu kinachokuja kusababisha
migogoro ya kugombea ardhi hivyo mpango huu utakuwa namanufaa makubwa kwa jimbo
hili la Mafinga Mjini” alisema Chumi
Aidha
Chumi alisema kuwa shule zilipata saruji hiyo ni shule mpya ya Maarifa nimekabidhiwa
mifuko 50 ya saruji sawa na nyingine ya Kinyanambo lakini pia nimetoa mifuko ya
saruji 30 kwa zahanati ya Rungemba lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa
wananchi.
Chumi
amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata za
ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za
jimbo la mafinga mjini.
Naye
mwenyekiti kata ya Changalawe Emmanuel Kuzugali ameelezea jinsi wananchi
walivyochangia kuwezesha ujenzi wa shule ya msingi utakaoanzishwa katika kata
hiyo.
Kwa upande wake diwani viti
maalumu kata ya changalawe Monica Luvanda ameelezea mchakato ulivyokuwa hadi
kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi wa shule ili kuendelea
kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo.
Comments
Post a Comment