- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Maendeleo Vijijini
on
- Get link
- X
- Other Apps
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini Blog
Septic mastitis ni maambukizi katika tezi za maziwa,
tezi ambazo zinatunga maziwa baada ya mnyama kuzaa.
Maambukizi haya hutokea wakati kunapokuwepo na ongezeko la
bacteria katika tezi za maziwa.
Kama tatizo hili litaachwa bila kutibiwa, bacteria wanaweza
kusambaa hadi kwenye damu na kwenye tezi za limfu, na kuathiri mwili mzima na
kuhatarisha maisha ya mnyama.
Kama maambukizi hayo yatabakia kwenye tezi za maziwa (mammary glands), usaha (abscess) unaweza kuonekana kwenye tezi hizo.
Uvimbe wa matiti (cystic
mastitis), ambao unatokana na maji yaliyojaa kwenye uvimbe, au vifuko vya
maji maji vilivyochukua nafasi ndani ya tishu za mwili, pia vinaweza kutokea
kwenye tezi na mirija ya tezi za maziwa (ambazo ni sawa na matiti ya binadamu).
Uvimbe huo huwa umejaa maji ya utasa au ugumba. Hali hii pia
inasababishwa na uvimbe mwingine kama huo kwenye mji wa uzazi na vifuko vya
mayai ya uzazi.
Kama hautatibiwa, uvimbe wa matiti unaweza kusababisha
saratani. Mara nyingi wanaoathirika zaidi ni sungura wenye umri wa kuzaa ama
wanyonyeshao.
Dalili na Aina
Uvimbe wa tezi za maziwa
* Kukosa hamu ya kula
(Anorexia), uchovu, kukosa
nguvu, kupungua uzito (lethargy), mfadhaiko
* Kupata kiu kubwa na
kukojoa sana (polydipsia, polyuria)
* Dalili za mimba
bandia (kama vile, kujinyonyoa manyoya, kujenga kiota cha kujifungulia, mimba
ya uongo)
* Kugua au kifo kwa
watoto.
Uvimbe wa matiti
* Mara nyingi mjanja, yuko makini sana,
hana maumivu
* Damu katika mkojo (hematuria),
ambayo mara nyingi inahusisha magonjwa kwenye mji wa uzazi
* Homan a kupungukiwa
maji.
Uchunguzi
Uchunguzi wa kawaida wa nje unaweza kuonyesha uvimbe mbichi,
mgumu, ulioiva, na tezi nyekundu za maziwa, na kuonekana kwa majimaji kwenye
matiti (ambayo siyo maziwa) kutoka kwenye tezi za matiti au chuchu.
Anaweza pia kuwa na homa kali pamoja na uchovu.
Uchunguzi wa kina wa damu unapaswa kufanyika, pamoja na
uchunguzi wa damu wa kikemia, kujua kiasi cha wingi wa damu, na kupima mkojo (urinalysis).
Vipimo hivi ndivyo vinavyoweza kubaini kama kuna maambukizi
yoyote.
Tiba
Kama maambukizi ni makubwa, ya kudumu, au yanajirudia, ni
vyema upasuaji ufanyike kuondoa tezi za matiti na vifuko vya mayai na mji wa
uzazi kwa afya ya sungura wako.
Kama maambukizi yatawahiwa mapema, na hayataonekana kuwa
katika kiwango kikubwa, dawa za maumivu za aina ya antibiotics ambazo ni maalum
kwa ajili ya bacteria waliomo zinaweza kutolewa kwa uangalifu mno.
Maisha na Matunzo
Unapaswa kudumisha mazingira wanamoishi sungura wako ili
kuzuia maambukizi mapya.
Kama sungura wako wamebainika kuwa na uvimbe wa tezi za
uzazi, na hali inajirudia ama ni ya kudumu, inashauriwa kuondoa tezi za matiti
kwa sababu uvimbe huo unaweza kuendelea na kuzaa kansa.
Imeandaliwa na www.maendeleovijijini.blogspot.com.
Tupigie: +255 656 331974
Comments
Post a Comment