Featured Post

VIJANA ZAIDI YA 60 WAMLALAMIKIA MUWEKEZAJI KWA KUWARUSHA FEDHA ZAO

 wamama wa kijiji cha Sambaru wakiendelea kutwanga mawe kwa ajili ya kuweka tayari kwa kupatikana madini ya  ya dhahabu.
Baadhi ya vijana wa kijiji cha Sambaru.

Na Woinde Shizza, Singida



Zaidi ya vijana 60 wa kijiji cha Sambaru kata ya Ikungi  wilayani Igungi mkoani Singinda wamemlalamikia mwekezaji wa kampuni ya  Sambaru  Gold Mining kwa kitendo cha kuwarusha fedha za malipo  ya kazi walikuwa wakimfanyia mgodini kwake

 Wakiongea na waandishi wa habari kijijini hapo baadhi ya vijana hao walisema kuwa wamefanya kazi katika kampuni hiyo kwa kipindi cha mda mrefu lakini muwekezaji huyo ajawalipa ela zao  na badala yake amewafukuza kazini hapo bila kuwalipa malipo yoyote .



Mmoja wa vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan alisema kuwa walishapeleka malalamiko yao kwa viongozi wa kijiji  lakini hakuna hatua  yeyote iliyochukuliwa hivyo wameiomba serikali iwasaidie ili wapate mafao yao kwani fedha hizo walikuwa wanazitegemea katika kuwasaidia katika majukumu mbalimbali ya kifamilia.



“tumekuwa tunamfata muwekezaji huyu na kumuomba  atulipe fedha zetu lakini amekuwa anatukana na kusema atudai ,mbaya zaidi kunawakati alifikia hatua ya kukamata baadhi ya wenzetu ambao wanamdai na kuwapeleka polisi,”alisema Saidi



Kwa upande wake kijana mungine aliyejitambulisha kwa jina la Fredy John alisema kuwa kunakipindi walishawahi kumpeleka polisi alipofika na kuulizwa kama vijana hao wanamdai alikuabali na akahaidi kuwalipa na aliomba mda na akapewa kimaandishi lakini ,muda huo umepita na hadi leo vijana hao awajalipwa na amefikia hatua ya kuwakana kabisa



Gazeti hili lilimtafuta mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sambaru Mfaume Hassan  ili kubainisha kama anataarifa za vijana hawa nae alisema kuwa ni kweli anataarifa za vijana hawa na alishamtumia mmiliki wa kampuni hiyo taarifa za kuwalipa vijana hawa lakini hajateleza   hivyo ameamua kupeleka swala hili katika ngazi za juu ili  wamsaidie



“sisi kama kijiji tumekuwa tuna utaratibu wa  kuwapa vijana wawekezaji hawa nah ii inatokana na uhitaji wa muwekezaji ,unakuta muwekezaji anataka vijana wa kumsaidia kazi uko mgodini kwake analeta barua katika ofisi ya kijiji  na sisi tunampa  vijana na ndio utaratibu uliofanywa sasa muwekezaji huyu kaja kuchukuwa vijana lakini cha kushangaza wamefanya kazi mgodini kwake lakini ajawalipa mpaka leo na mbaya zaidi akifatwa anasema kuwa adaiwi kitu ambacho sio cha kweli mimi kama kiongozi wa kijiji nikishirikiana na wenzangu tutajitaidi kufuata sheria ili vijana hawa walipwe ela zao na hadi sasa navyoongea nilishampa taarifa mkuu wa wilaya”alisem Mwenyekiti wa kijiji Mfaume Hassan



Gazeti hili lilimtafuta  mmiliki wa kampuni ya Sambaru  Gold Mining Ahamed Magoma  kujibu  tuhuma hizi nae alisema kuwa yeye kama yeye adaiwi na kijana yeyote Yule wa kijiji cha Sambaru ,na kama kuna mtu anae mdai afuate  vyombo husika vya sheria akamdai



“mimi sidaiwi na kijana yeyote Yule vijana wangu wote ambao nawaajiri  nawalipa vizuri na wengine wapo kazini hadi sasa,pia mimi sijawai kwenda kijijini kutafuta kijana wa kunifanyia kazi na napenda kusema ivi kama kuna mtu ambae ananidai afuate sheria  ,aje na vielelezo anidai  na kama ni kweli nitamlipa ila sidaiwi na mtu yeyote “alisema Magoma



Akiongelea swala hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu alisema kuwa swala hilo alishalipokea kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji cha Sambaru  na alimuagiza aandike idadi ya vijana hao pamoja na majina yao ili ayafanyie kazi ,aidha pia alisema kuwa atamuandikia barua  ya kumuita ofisini kwake  mmiliki wa mgodi huo wa Sambaru Gold Mining .



Comments