- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na Mtendaji
Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga, wakati
alipotembelea Mfuko huo, jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mfuko
wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Eng. Peter Ulanga, akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, namna Mfuko huo
unavyohakikisha mawasiliano ya simu na data unapatikana hususan vijijini, jijini
Dar es Salaam.
Baadhi ya watendaji wa
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo pichani), wakati
alipowatembelea na kuzungumza nao changamoto na namna ya kufanikisha malengo ya
Mfuko huo, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akizungumza na uongozi wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), kuhusu uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini
leo, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), Bw. Salim Msangi akitoa taarifa ya utendaji
wa Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani, wakati alipokuwa akizungumza nao leo, jijini Dar es Salaam.
Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Serikali imeutaka
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), kuona namna ya kuboresha huduma za mawasiliano
ya simu na data vijijini ili kuwawezesha wananchi kufikiwa na huduma hiyo
kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi
wa habari katika ofisi za Mfuko huo jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, amesisitiza kwa
Mfuko huo kuhakikisha unafikisha mawasiliano katika maeneo ambayo hayajafikiwa
na huduma hiyo kabisa lengo likiwa ni kufanya usawa na kuwezesha vijiji vyote
kufikiwa na huduma hiyo.
"Hakikisheni
mnapeleka mawasiliano katika vijiji ambavyo hakuna mawasiliano kabisa kwani
wananchi wamekuwa wakilalamika kutofikiwa na huduma", amesema Naibu Waziri
Ngonyani.
Aidha, ameutaka
Mfuko huo kuwasimamia watoa huduma nchini kuhakikisha wanafunga minara na
mitambo sahihi katika maeneo mbalimbali nchini ili kuepusha usumbufu kwa
wananchi.
Ameutaka Mfuko
huo kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufanya ukaguzi wa
mara kwa mara ili kuhakikisha maeneo ambayo watoa huduma wamejenga minara
yanakuwa ni ya uhakika.
Ameongeza kuwa
Mfuko huo una wajibu wa kutafuta vifaa vingine vitakavyowawezesha kusaidia
kufanya ukaguzi kwa haraka badala ya kukaa na kusubiri vifaa vya TCRA.
Ametoa rai kwa
makampuni ya simu nchini hususan yanayochangamkia zabuni za Serikali kupitia
mfuko huo kutoa taarifa sahihi za usimikaji wa minara na utendaji wake kwa
mfuko huo ili kusaidia kuboresha mawasiliano vijijini kwa nia moja.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Eng. Peter Ulanga, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa wataendelea kuwasimamia watoa huduma nchini kuhakikisha wanajenga minara na kuhakikisha inafanya kazi masaa yote.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Ngonyani ametembelea Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), na kuwasisitiza kuwajibika katika kuongeza mapato na kuendelea na uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini ili kukuza sekta ya usafiri wa anga.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Eng. Peter Ulanga, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa wataendelea kuwasimamia watoa huduma nchini kuhakikisha wanajenga minara na kuhakikisha inafanya kazi masaa yote.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Ngonyani ametembelea Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), na kuwasisitiza kuwajibika katika kuongeza mapato na kuendelea na uboreshaji wa viwanja vya ndege nchini ili kukuza sekta ya usafiri wa anga.
Naibu Waziri
ameendelea na ziara yake ya kikazi jijini Dar es Salaam ambapo ametembelea na
kuzungumza na uongozi wa UCSAF na TAA.
Comments
Post a Comment