Featured Post

TIB CORPORATE BANK KTK JUKWAA LA BIASHARA TANGA

 Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Dokta Harrison Mwakyembe kulia akilakiwa na wajumbe wa Jukwaa hilo wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TSN Dokta Jimmy Yonazi wanne kushoto ni MD wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege na wakwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.



TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara ,Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta maendeleo.
 
TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali KTK Mkoa wa tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities).
 
TIB Corporate Bank  inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati,dhamana za kibenki( bank guarantee),ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni,uwekezaji katika hati fungani,( treasury bills & Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka
  
Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.

Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

Comments