- Get link
- X
- Other Apps
Featured Post
RAIS DKT. MAGUFULI AAGANA NA MGENI WAKE RAIS WA MISRI PIA AKUTANA NA WAZIRI WA ZAMANI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN
Posted by
Unknown
on
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati wa
nyimbo za mataifa mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere(JNIA). Rais huyo wa Misri ameondoka mara baada ya kumaliza ziara
yake ya siku mbili hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsindikiza mgeni wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi wakati akielekea
kupanda ndege mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kumaliza ziara
yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akicheza nyimbo za kikundi cha matarumbeta kilichokuwa kikitumbuiza katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara baada ya kumsindikiza mgeni
wake Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza
ziara yake ya siku mbili nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana
na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa aliyefika
Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika mazungumzo na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan
Ichiro Aisawa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Mbunge na Waziri wa zamani wa Mambo ya nje wa Japan Ichiro Aisawa
mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Comments
Post a Comment